Bocco aiangamiza Simba na kuisafishia njia Yanga
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Mshambuliaji John Raphael Bocco ameipa ushindi Azam wa bao 1-0 ikiilaza Simba SC na kusitisha kabisa ndoto za Wanamsimbazi kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi.
Simba leo imecheza kandanda safi na kuonekana kuwamudu kabisa Azam ambao walisubiri hadi kipindi cha pili kuandikisha bao la ushindi ambalo sasa linawafanya Simba kusalia kileleni kwa masaa tu kwani kesho Yanga akishinda atakwea kileleni.
Hadi mapumziko timu zote mbili zilienda vyumbani vikiwa havijafungana, beki Mzimbabwe Method Mwanjali ambaye amezoa tuzo mbili za uchezaji bora wa mwezi Desemba akianzia katika klabu yake ya Simba na ile ya wadhamini wa Ligi Kuu, Vodacom leo amebugi stepu kwa kumpa nafasi Bocco kuiangamiza Simba kinyama