Mtibwa yaibana koo Simba
Na Ikram Khamees, Morogoro
Simba SC ya Dar es Salaam jioni ya leo imeshindwa kuchomoza na ushindi baada ya kulazimishwa sare isiyo na mabao 0-0 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kukaa kileleni ikifikisha pointi 45 ikiongoza kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya hasimu wake mkuu Yanga SC ambao jana walishinda 1-0 dhidi ya Majimaji ya Songea.
Mchezo wa leo ulikuwa mkali ambapo kila timu ikicheza vizuri lakini ngome ya ulinzi ya Mtibwa iliyokuwa ikisimamiwa vema na Henry Joseph iliwazuia kabisa washambuliaji wa Simba waliokuwa wakiongozwa na Mrundi Laudit Mavugo