Rasmi: Jesus kucheza Man City
Klabu ya Manchester City ya England imepata idhini ya kumnunua rasmi winga wa Kibrazil mwenye umri wa miaka 19 Gabriel Jesus na sasa anaweza akacheza dhidi ya Tottenham Jumamosi ijayo.
Jesus amehamia City kutoka Klabu ya Palmeiras ya Brazil kwa £27m. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil alikubali kuhamia City kwa mkataba wa miaka mitano Agosti mwaka jana.
Alisalia na Palmeiras hadi mwisho wa msimu wa soka Brazil mwezi Desemba. Jesus ana uwezo wa kuibuka kuwa miongoni mwa washambuliaji bora zaidi katika soka, mkurugenzi wa soka wa City Txiki Begiriatain amesema