TIP TOP CONNECTION KWISHINEI

Na Saida Salum, Dar es Salaam

Kundi lililojipatia umaarufu mkubwa katika muziki wa kizazi kipya lililokuwa na maskani yake Manzese Tip Top jijini Dar es Salaam limesambaratika rasmi na kila msanii ameamua kufanya muziki huru.

Akizungumza na Mambo Uwanjani, Aliyekuwa kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally "Madee" amesema mwisho wa Tip Top Connection umefika na sasa ni wakati wa kila msanii kufanya muziki kivyake 'Solo Artist, alisema Madee.

Msanii huyo aliyetamba na nyimbo mbalimbali zilizopata kutambulika ndani na nje ya nchi, ameendelea kusema muziki wa kundi haulipi na ni bora msanii kujitegemea, Lakini inasemekana kusambaratika kwa kundi hilo kumetokana meneja wao Babu Tale kunogewa na Diamond Platinumz na kuamua kuachana na kundi hilo ambalo halimlipi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA