Simba yapeta rufaa ya Lufunga
Na Prince Hoza, Dar es Salaam
Klabu ya Simba imepeta rufaa yake iliyokatiwa na Polisi Dar baada ya kumjumuhisha mchezaji wake Novat Lufunga katika mchezo wa michuano ya kombe la Azam Sports Federatipn Cup ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.
Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na Simba kudanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ulipelekea rufaa kwa timu ya Polisi Dar ikitaka ipewe ushindi kufuatia Simba kumtumia mchezaji mwenye kadi nyekundu aliyopewa mwaka jana kwenye michuano kama hiyo.
Lufunga alipewa kadi nyekubdu wakati Simba ilipocheza na Coastal Union, lakini Kamati ya Mashindano ya TFF iliyokutana leo imeitupilia mbali rufaa hiyo na kusema Simba haikuwa na kosa lolote kumtumia mchezaji huyo kwani michuano ya mwaka jana si ya mwaka huu.
Alfred Lucas ambaye ni Afisa Habari wa Shirikisho hilo amesema Simba ilikuwa na haki ya kumtumia Lufunga na Polisi Dar haiwezi kupewa ushindi wowote, hata hivyo Polisi Dar haikutimiza vigezo vya uwasilishaji rufaa kwani hawakulipa ada