Okwi atemwa Denmark, yadaiwa ameshuka kiwango

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mshambuliaji Mganda Emmanuel Anord Okwi ameamua kuondoka nchini Denmark, Okwi amevunja mkataba wake na Klabu ya Sonderjske Fodbold ambayo alijiunga nayo akitokea Simba.

Mkuu wa masuala ya michezo ya Klabu hiyo, Jorgen Hayson amesema Okwi mwenye umri wa miaka 24 ameamua kuvunja mkataba baada ya kuona hajapata namba ya uhakika katika kikosi hicho.

"Okwi hakupata nafasi ya kucheza kama ambavyo alitarajiwa lakini kiwango chake pia hakikukua kumshawishi kocha aanze kumpa nafasi kwa kiwango cha juu", alisema na kuongeza.

"Mwisho akaamua kuondoka, tumekaa na kufikia makubaliano vizuri, zaidi ninamtakia kila la kheri aendako, alisema. Okwi alitua katika kikosi hicho Julai 2015 akitokea Simba na kusaini mkataba wa miaka mitano na mkataba wake ungeisha mwaka 2020.

Hata hivyo mara kwa mara Okwi amekuwa akihusishwa kurejea Simba lakini amekuwa haeleweki, mara kadhaa amekuwa akikanusha na mara nyingine akieleza yuko tayari kuzungumza au yujo tayari kurejea Simba.

Hata hivyo viongozi wa Simba wamekuwa kwenye mgawanyiko mkubwa kuhusiana na ujio wake, wako wakitaka arejee na wengine wakipinga kabisa

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA