Simba kwameguka
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
Katibu mkuu wa Klabu ya Simba Patrick Kahemele ameachia ngazi na kuamua kurejea Kampuni ya Bakhressa Group Limited.
Kahemele aliyekuwa katibu wa Simba tangu Juni mwaka jana anarejea Bakhressa Group kwenda kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Azam TV nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Charles Hilary.
Gwiji wa habari Charles Hilary sasa anakwenda kuwa Mkurugenzi mtayarishaji wa vipindi vya Azam TV. Katika kipindi chake kifupi cha kufanya kazi Simba Kahemele alionyesha dira ya mabadiliko kabla ya kuondoka ghafla na kurejea Azam.
Wazi kuondoka kwa Kahemele aliyeibukia Mtibwa Sugar na baadaye akawa meneja wa Azam FC na mwasisi wa Azam TV ni pengo kwa Simba. Bila shaka mjumbe wa kamati ya utendaji Collin Frisch atarejea kukaimu nafasi hiyo wakati Klabu ikitafuta mtu mwingine