Majimaji na Yanga nani kucheka leo?
Na Salum Fikiri Jr, Songea
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga SC, jioni ya leo wanashuka Uwanja wa Majimaji mjini Songea kuwavaa wenyeji wao 'Wana Lizombe' Majimaji mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).
Majimaji inayonolewa na Kally Ongala mchezaji wa zamani wa mabingwa hao watetezi na Azam FC, Mchezo huo utakuwa wa kisasi kwani Majimaji ilifungwa mabao 3-0 na Yanga zilipokutana Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.
Hivyo leo Majimaji inataka kulipiza kisasi na pia inataka kujinusuru kutoka mkiani, Yanga nao wanataka kuendeleza ubabe kwa Majimaji lakini pia inataka kuwapa furaha mashabiki wake baada ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi huko Zanzibar na kikubwa zaidi wanataka kuwapoza mashabiki wao.
Kwa vypvyote pambano litakuwa kali na la kusisimua, Yanga waliwasili mjini Songea Jana jioni wakipitia Tunduru kwa basi ambako walipata mapokezi makubwa toka kwa mashabiki wao