MISRI, GHANA ZAPETA AFCON

Goli lililofungwa na Mahmoud Kahraba dhidi ya timu ya taifa ya Morocco limeivusha timu ya taifa ya Misri katika Nusu fainali ya mashindano ya Afcon 2017.

Mtanange huo uliopigwa kwenye uwanja wa Stade de Port Gentil usiku hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa hazijafungana. Bao lililoipatia ushindi Misri limefungwa dakika ya 88 ya kipindi cha pili ikiwa ni dakika 2 kabla kipyenga cha dakika 90 kupulizwa.

Kwa matokeo hayo, Misri sasa itakutana na Burkina Faso katika hatua ya nusu fainali. Wakati Misri wakitinga hatua hiyo, Ghana nao walikuwa wa kwanza kufuzu nusu fainali jioni baada ya kuiadhibu DR Congo kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua.

Andre Ayew na mdogo wake Jordan Ayew ambao ni watoto wa Abedi Pele gwiji la zamani la soka barani Afrika walifunga bao moja kila mmoja na kuisaidia Ghana kushinda mchezo huo mechi ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya Afcon nchini Gabon.

Ghana sasa itakutana uso kwa uso na ndugu zao wa Cameroon mchezo ambao utaamua nani asonge fainali ya mwaka huu na mwishowe kumpata bingwa wa Afrika

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA