Burkina Faso yatangulia nusu fainali Afcon, Cameroon nao kimeeleweka
Timu ya taifa ya Burkina Faso imefanikiwa kuingia nusu fainali ya mataifa ya Afrika baada ya kuendeleza ubabe kwa Tunisia ikiwalaza mabao 2-0.
Kwa maana hiyo Burkina Faso unasubiri mshindi kati ya Misri na Morocco ambazo zinaumana Jumapili, Simba wasiofungika Cameroon nao walifanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuilaza Senegar kwa mikwaju ya penalti 5-4.
Miamba hiyo ya Afrika yenye rekodi ya kutinga robo fainali ya kombe la Dunia zilimaliza dakika 90 zikiwa 0-0 na katika mikwaju ya penalti Cameroon iliibuka mshindi na hasa kipa wake Joseph Ondoa akistahili pongezi baada ya kuokoa penalti ya Senegar.