Uwanja wa Taifa sasa ruksa Ligi Kuu
Na Saida Salum, Dar es Salaam
Serikali imeuruhusu uwanja wa Taifa uliopo Temeke jijini Dar es Salaam kutumika kwa shughuri za michezo ikiwemo soka.
Taarifa ya ruhusa ya uwanja huo imetolewa na Wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na wasanii na Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Magufuli ndiye aliyetoa msamahs kwa uwanja huo ambao ulifungiwa.
Kwa maana hiyo mechi ya kesho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba na Azam itachezwa kwenye uwanja huo, ikumbukwe mashabiki wa Simba ndio waliosababisha uwanja huo kufungwa baada ya kufanya vurugu kwa kung: oa viti walipocheza na mahasimu wao Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu