Yanga na Ashanti kumenyana leo FA Cup
Na Sharifu Sharifu, Dar es Salaam
Mabingwa watetezi wa kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, Yanga SC jioni ya leo wanaanza kampeni yao ya kutetea taji lao itakaposhuka uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuumana na Wauza Mitumba wa Ilala Ashanti United.
Mchezo huo unatazamiwa kuwa mkali kutokana na timu zote kupokea ratiba ya michuano hiyo ghafla, Ashanti haipewi nafasi kubwa ya kuifunga Yanga kwakuwa ni timu ya daraja la kwanza, lakini inaweza kufanya miujiza na kuchomoza na ushindi.
Yanga nao wanauchukulia mchezo huo kama njia ya kuelekea kwenye ushiriki wa michuano ya Shirikisho mwakani, kesho Simba SC itacheza na Polisi Dar katika uwanja huo huo wa Uhuru