Shekhan Rashid apiga bao lingine Sweden
Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Thomas Ulimwengu akienda nchini Sweden kucheza soka la kulipwa katika Klabu moja ya Ligi Kuu, kiungo wa zamani wa Simba Shekhan Rashid yeye ameongeza mtoto wa tatu.
Shekhan yupo Sweden baada ya kuachana na soka la ushindani akaamua kuchukua uraia na kujikita kwenye maisha ya familia na hivi majuzi tu mkewe amejifungua mtoto (Pichani) akiwa na afya njema.
Hongera Shekhan Rashid