Ni mechi ya kisasi Simba Vs Azam
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam
Leo ndio leo asiye na mwana abebe jiwe, vinara wa Ligi Kuu Bara Simba SC jioni ya leo wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kukwaruzana na Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotazamiwa kuwa mkali.
Mchezo huo utakuwa mkali kutokana na miamba hiyo kutoka kuumana hivi karibuni katika fainali ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar na Azam kushinda 1-0.
Simba wanaingia katika mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu lakini wakitaka kulipiza kisasi baada ya kulala kwenye fainali, kwa upande wa Azam nao wanataka kushinda mchezo huo ili kulipiza kisasi kwani katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara walilala 1-0.
Azam itawategemea zaidi nyota wake John Bocco 'Adebayor', Salum Abubakar, Himid Mao Mkami, Yahaya Mohamed na Stephano Kingue Mpongou, Simba nao watamtegemea zaidi Shiza Kichuya, Ibrahim Ajibu, Mohamed Ibrahim, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo.
Endapo Simba itashinda mchezo huo itaendelea kukalia usukani kwa kufikisha pointi 47 na kama ikifungwa ama kutoka sare basi Yanga anaweza kukamata usukani endapo kesho ataifunga Mwadui