WENGER AFUNGIWA MECHI NNE
Mkufunzi wa Arsenal Arsenel Wenger amepigwa marufuku ya mechi nne na faini ya pauni 25,000 baada ya kukiri mashitaka ya FA kwa tabia yake mbaya katika mechi dhidi ya Burnley.
Wenger mwenye umri wa miaka 67 alishitakiwa kwa kumtusi na kumsukuma msaidizi wa refa Anthony Taylor baada ya kutakiwa kutoka uwanjani.
Marufuku yake inaanza mara moja kwa hivyo atakosa mechi ya FA dhidi ya Southmpton. Iwapo mechi hiyo italazimika kurudiwa, Wenger atarudi uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Uingereza dhidi ya Hull City mnamo tarehe 11 mwezi Februali.
Hata hivyo iwapo mechi hiyo itakamilika siku ya Jumamosi na mshindi kubainika mechi dhidi ya Hull City itakuwa mechi yake ya nne na ya mwisho kuhudumia marufuku hiyo kufuatia mechi dhidi ya Watford na Chelsea