Baloteli abaguliwa Ufaransa

Mshambuliaji wa timu ya Nice nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiliwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia.

Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 alichapisha katika mtandao wa kijamii akisema ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua.

"Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu, ni aibu kubwa'.

Balotelli alicheza dakika 90 aluporudi uwanjani baada kuhudumia marufuku katika mechi iliyotoka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram uliosambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo.

Jopo la adhsbu la Ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote, Balotelli amefunga mabao 10 katika mechin15 tangu kujiunga na Nice katika uhamisho huru kutoka Liverpool mwezi Agosti miaka miwili baada ya uhamisho wa pauni milioni 16 kuelekea Anfield

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA