Nyosso apigwa marufuku mchangani
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam
Nahodha wa zamani wa Mbeya City, Juma Said Nyosso amezuiwa kucheza katika michuano ya Asenga Diwani Cup inayofanyika Uwanja wa Shule ya msingi Tabata.
Nyosso ambaye pia amewahi kuzichezea Ashanti, Simba na Coastal Union amejikuta akizuiwa kushiriki michuano hiyo ya mchangani ni kutokana na kamati inayoandaa michuano hiyo kuheshimu maamuzi ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) ambalo limemfungia mchezaji huyo.
TFF ilimfungia Nyosso baada ya kudaiwa kumshika makalioni nahodha wa Azam John Rafael Bocco, beki huyo aliyeibukia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys chini ya umri wa miaka 17 alifungiwa kwa muda wa miaka miwili adhabu ambayo itamalizika msimu ujao.
Mchezaji huyo aliichezea timu ya Matumbi FC ya Tabata ambapo aliiwezesha kutwaa Ng' ombe mnyama katika michuano iliyopita, lakini hii ya Diwani Cup Nyosso amezuiwa kwa madai ana adhabu hivyo hapaswi kucheza