Simba yamtosa Okwi kisa kiwango

Na Saida Salum, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka bayana kwamba hawana mpango wa kumsajili mshambuljaji wake wa zamani Emmanuel Anord Okwi raia wa Uganda mpaka pale itakapojiridhisha na kiwango chake.

Mwenyekiti wa kamati ya usajilj Zacharia Hanspoppe amesema hayo hasa baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Simba inataka kumrejesha mchezaji wake huyo wa zamani ambaye amevunja mkataba wake na Klabu ya Sonderjyjske ya Denmark.

Okwi amevunja mkataba na Klabu hiyo ya Ligi Kuu baada ya kutokuwa na uhakika wa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza hivyo akaona ni bora aondoke zake, Lakini meneja wa michezo wa Klabu hiyo akasema Okwi alisajiliwa kutoka Simba kwa lengo la kuisaidia timu hiyo lakini kiwango chake hakijawaridhisha na ndio maana kocha wa timu hiyo alikuwa hamtumii.

Hanspoppe amedai kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha Msimbazi hadi pale watakaporidhishwa na kiwango chake na hawatamtumia msimu huu labda ujao, Hanspoppe amewataka Wanasimba kutulia na kuachana na uzushi unaoenezwa sasa kuhusu nyota huyo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA