Ni kivumbi na jasho Simba na Mtibwa
Na Ikram Khamees, Morogoro
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba SC jioni ya leo inakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Simba wataingia katika mchezo huo ikiwa na lengo moja la kushinda mchezo huo ili iweze kufufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa bara baada ya kushindwa kuutwaa kwa muda wa miaka minne mfululizo.
Endapo itashinda katika mchezo huo itafikisha pointi 47 na kuzidi kuiacha Yanga iliyo katika nafasi ya pili na pointi 43, lakini Mtibwa Sugar wanaonolewa na Salum Mayanga wametamba kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Mtibwa inawategemea zaidi Shaaban Mussa Nditi, Haroun Chanongo na Rashid Mandawa wakati Wekundu wa Msimbazi nao tumaini lao lipo kwa Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim 'Mo'