Ghana yainyuka Mali na kutinga robo fainali, Uganda out
Ghana imefuzu hatua ya robi fainali ya michuano ya mataifa Afrika baada ya jana kuilaza Mali bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa saa 12 jioni katika dimba la Stade de Gentil Libraville Gabon.
Kwa matokeo hayo yanaifanya Ghana ifikishe pointi sita na kutinga hatua ya robo fainali, mchezo mwingine uliopigwa katika uwanja huo huo saa 3 usiku timu ya taifa ya Misri iliichakaza Uganda bao 1-0.
Wafungaji wa magoli katika mechi zote, Asamoah Gyan aliifungia Ghana bao LA ushindi, wakati Abdallah Said naye aliipatia Misri bao pekee la ushindi, Uganda sasa wamefungasha virago hasa baada ya kupoteza mechi zote mbili mfululizo na sasa watasaliwa na mechi ya kukamilisha ratiba