Ghana yaichapa Uganda Afcon
Timu ya taifa ya Ghana 'Black Stars jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kutwaa ubingwa wa mataifa ya Afrika baada ya kuilaza bao 1-0 timu ya taifa ya Uganda 'The Cranes' katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika nchini Gabon.
Iliwachukua Ghana kupata penalti iliyowekwa kimiani na Andwer Ayew na kuipa ushindi nchi yake ambayo sasa inaongoza kwenye kundi lake ikiwa na pointi 3, Misri na Mali zitaumana katika mchezo mwingine unaofuata.
Farouk Miya nusura aisawazishie bao Uganda lakini jitihada zake zilishindikana na hadi mwisho wa mchezo Ghana washindi wa pili wa mataifa ya Afrika iliyopita wametoka kidedea kwa ushindi huo mdogo dhidi ya watoto wa Yoweri Museveni