YAYA TOURE AKATAA MAMILIONI YA WACHINA
Kiungo wa kati wa Klabu ya Manchester City Yaya Toure amekataa ombi la mshahara wa pauni 430,000 kwa wiki kutoka China.
Toure mwenye umri ws miaka 33 amevutia timu nyingi katika ligi ya China wakati ilipoonekana kwamba huenda asishirikishwe katika mechi zozote chini ya mkufunzi Pep Guardiola.
Aliamua kutoondoka wakati huo na akakatas tena alipopewa kitita hicho wakati wa dirisha hili la uhamisho, kandarasi ya raia huyo wa Ivory Coast inakamilika mwishoni mwa msimu huu.
Toure amekuwa mchezaji muhimu wa City tangu aliporudishwa katika kikosi cha kwanza na alianza mechi yake ya saba mfululizo wakati wa kushindwa kwa mabao 4-0 dhidi ya Everton katika ligi ya Uingereza hapo Januari 15 mwaka huu.
Nyota huyo yuko huru kuingia mkataba na klabu yoyote ughaibuni tangu Januari lakini imedaiwa kwamba bado anaipenda ligi ya Uingereza na timu yake ya City, Toure hajapata hakikisho lolote kugusu kandarasi kutoka kwa kocha wake Guatdiola