Misri yaibutua Ghana lakini zote zafuzu robo fainali

Michezo miwili ya mwisho ya hatua ya makundi ya michuano ya Afcon 2017 imemakizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ghana na hivyo kuongoza kundi D kwa alama 7 huku Ghana wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.

Bao la ushindi la Mafarao wa Misri lilifungwa na nyota wao Mohamed Salah, katika dakika ya 11 ya mchezo kwa mkwaju mkali wa mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja nyavuni..

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo rimu ya Uganda walitoshana nguvu na Mali kwa kufungana bao 1-1. Michezo ya hatua ya robo fainali itaanza kuchezwa Jumamosi ya Tarehe 28 kwa Burkina Faso kucheza na Tunisia huku Senegar wakicheza na Cameroon.

Jumapili kutachezwa michezo miwili ya robo fainali ya pili kwa DR Congo kuchuana na Ghana nao Misri wakikipiga na Morocco ni vita ya Waarabu kwa Waarabu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA