Ivory Coast wavuliwa ubingwa wa Afrika, DR Congo wapeta
Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Tembo wa Afrika Ivory Coast wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa bao 1-0 na Simba wa Astlas Morocco.
Goli pekee lililowaondoa miamba hao wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.
Nayo timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliitambia Togo kwa kuichapa mabao 3-1 na hivyo kufuzu robo fainali wakiwa vinara wa kundi C kwa alama 7 huku Morocco wakishika nafasi ya pili kwa pointi 6.
Morocco na DR Congo wamefuzu kupitia kundi hilo huku Ivory Coast na Togo wameondoshwa rasmi