Malinzi aula Fifa
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa miguu ulimwenguni (FIFA) limemteua Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Jamal Emily Malinzi kuwa mjumbe maalum wa kamati ya maendeleo ya soka duniani.
Malinzi sasa atakuwa na jukumu la kuendeleza soka duniani kama.afanyavyo hapa nchini, hii imekaa njema kwa kiongozi wa mpira wa miguu nchini, Malinzi atahudumu katika nafasi hiyp kwa miaka mitano.
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani (Fifa) Gian Infatinho amesema Malinzi ni mtu muhimu katika maendeleo ya mpira wa miguu duniani na kwa jitihada zake anaweza kuisaidia kamati hiyo kufikia malengo yake