Serena Williams amgalagaza dadake

Serena Williams amedhihirisha kuwa yeye ndio mbabe wa Tennis duniani kwa sasa baada ya kumshinda dadake Venus Williams na kutwaa taji lake la saba la Australia Open na kuweka rekodi ya Opera kwa kushinda mataji 23 ya Grand Slam.

Serena mwenye umri wa miaka 35 alishinda katika seti za 6-4, 6-4 ili kumpiku Steffi Graf katika orodha ya washindi wakuu tangu Grand Slam kuwakubali wachezaji wa kulipwa 1968.

Raia huyo wa Marekabi sasa ataorodheshwa wa kwanza duniani kwa kumpiku aliyekuwa mchezaji nambari moja upande wa wanawake Angelique Kebber kutoka Ujerumani.

Raia wa Australia Margeret Court ndiye mchezaji pekee ambaye yuko mbele ya Serena baada ya kushinda mataji 24 ya Grand Slam

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA