Simba yawatafuna Polisi Dar

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Wekundu wa Msimbazi Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dar Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup.

Ushindi wa Simba ni sawa na ule wa Yanga uliochezwa jana ambapo waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ashanti, hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao moja lililowekwa kimiani na mshambuliaji wake Pastory Athanas.

Kipindi cha pili Simba waliongeza bao la pili lililofungwa na Mohamed Hussein Zimbwe Jr au Tshabalala, kwa maana hiyo Simba imeungana na Yanga kutinga hatua ya 16

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA