Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

MICHANO: ZAY B MWANADADA GAIDI ALIYENASWA KIZEMBE NA SISTA P

Picha
Na Mkola Man, TANGA Yap...yap....yap. michano ya leo inamchana mwanahip hop wa kwanza wa kike hapa bongo Zainabu Lipangile maarufu Zay B aliyetamba na wimbo wake uitwao 'Gado' aliomshirikisha Inspekta Haroun 'Babu' na remix yake alimshirikisha Juma Nature. Zay B mwanadada gaidi, gaidi aliyekamatwa na Sister P ambaye alikuwa pandikizi la kumshusha Zay B, alichokosea Zay B wakati anakimbizwa, alisimama akijifanya yeye ni gaidi. Laiti kama angekimbia asingekamatwa na Sister P na ndio maana waswahili husema ukikimbizwa usigeuke nyuma, utajikwaa, ushauri wangu kwa rapa Zay B kipaji hakizeeki kisha ajue kutofautisha kukaa na kuchuchumaa. Mashabiki wake bado wapo, Michano ya Mkola Man lengo ni kujenga na si kubomoa, Tukutane wiki ijayo siku kama ya leo, je unataka tumchane nani 0715281223 Zay B mwanadada gaidi aliyekamatwa kirahisi na Sister P

AZAM FC YAPIGA WANAJESHI 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM Mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kuzima ngebe za maafande wa Prisons ya Mbeya baada ya ouwatandika mabao 3-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam. Ushindi huo unawapeleka Azam Fc hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Azam Sports Federation Cup maarufu kama kombe la FA Cup. Shomari Kapombe aliifungia Azam mabao mawili wakati Hamisi Mcha akifunga moja na kufanya Azam iibuke na ushindi mnono, bao la kufutia machozi la Prisons lilifungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah Juma Mgunda. Hata hivyo mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kwani timu hizo zinapokutana huwa zinakamiana sana, mara ya mwisho kukutana ilikuwa jijini Mbeya uwanja wa Sokoine mchezo wa ligi kuu bara ambapo zilitoka sare ya kufungana 1-1 Azam Fc jioni ya leo imewachapa maafande wa Prisons

NANI KAKWAMBIA KIPORO KINACHACHA KWA YANGA, YAIKANDIKA 2-1 NDANDA, YATINGA NUSU FAINALI

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo imeichapa timu ya Ndanda Fc ya Mtwara mabao 2-1 katika uwanja wa Taifa Dar ea Salaam mchezo wa robo fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup. Yanga wakicheza kwa taadhali kubwa walijipatia bao la kuongoza kunako dakika ya 35 kipindi cha kwanza likifungwa na mshambuliaji wake Poul Nonga ambaye leo amecheza vizuri. Hadi mapumzikp Yanga walikuwa mbele kwa goli hilo, kipindi cha pili timu zote zilirudi uwanjani na Ndanda walionekana kucharuka wakitaka kusawazisha bao hilo, iliwachukua muda mfupi baadaye Kiggi Makassy winga wa zamani wa Yanga na Simba aliisawazishia Ndanda na kuwa moja kwa moja. Poul Nonga kwa mara nyingine alimpa pasi nzuri Simon Msuva ambaye alikuwa anaingia na mpira langoni mwa Ndanda kabla ya beki Poul Ngalema kumkwatua na mwamuzi kuipa penalti Yanga. Mwamuzi huyo pia alimpa kadi nyekundu mchezaji huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Simba na kuwafanya Ndanda kucheza pung...

MABAGA FRESH WARUDI NYUMBANI KIAINA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM Kundi la muziki wa kufokafoka lililowahi kujipatia umaarufu mkubwa miaka iliyopita la Mabaga Fresh hatimaye wameamua kurudi nyumbani baada ya kimya kirefu. Akizungumza na mtandao huu, Dj Snox mmoja kati ya wasanii waounda kundi hilo amesema wameamua kurudi nyumbani kwa maana wanaachana na muziki wa Kimarekani na kugeukia muziki wa Kiafrika. "Tumerudi nyumbani, ndio wimbo wetu mpya tuliouimba kwa mtindo wa Kinanda na Singeli, tumeachana na kopi za Kimarekani kwani mitindo ya Hip Hop na Bongofleva ni za Kimarekani", alisema. Kundi hilo lililotamba na nyimbo zake kama "Mabaga Fresh tuko kamili", "Mtulize" na nyinginezo ambazo walishirikiana na Juma Nature

YANGA VS NDANDA TAIFA, AZAM NA PRISONS CHAMAZI, HAPATOSHI LEO FA CUP

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikabili Ndanda Fc ya Mtwara mchezo wa robo fainali kombe la Azam Sports Federation Cup au FA Cup. Mchezo huo unatazamiwa kuanza saa kumi jioni na utakuwa mkali wenye ushindani hasa kila timu ikitaka kucheza nusu fainali, tayari timu ya Mwadui Fc ya mjini Kahama imeshatangulia nusu fainali. Mwadui ilipata tiketi hiyo baada ya kuilaza Geita Gold ya Geita mabao 3-0, mchezo mwingine unatarajia kufanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kati ya mabingwa Afrika mashariki na kati maarufu kbe la Kagame Azam Fc itachuana na Prisons ya Mbeya. Mchezo huo nao utakuwa mkali kutokana na timu hizo kuonyeshana undava kila zinapokutana Amissi Tambwe wa Yanga akikabiliana vikali na mlinzi wa Ndanda wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni

HE! CHIFU PANDUKA ANAUNGANISHA WATU KWENYE FREEMASON, WASANII, WANASIASA WAMIMINIKA KWAKE

Picha
Na Juma Mwema, DAR ES SALAAM Mganga na mnajimu wa nyota Afrika mashariki na kati Chifu Panduka inasemekana anaunganisha watu kwenye mtandao wa freemason na pia amekuwa akitoa pete ambayo hung' arisha nyota zao. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata na zenye uhakika kwamba mnajimu huyo amekuwa akiwaunganisha watu mbalimbali na imani hiyo inayoaminika kuwa ya nguvu za giza huku akiwaaminisha kwamba watapata utajiri. Mwandishi wetu aliyekuwepo katika kituo cha mnajimu huyo kilichopo Tabata relini Dar es Salaam ameshuhudia mastaa mbalinbali wa muziki, sanaa na wanamichezo wakimiminika kwake. Pia wafanyabiashara maarufu na viongozi wa siasa nao wamekuwa wakifika kwa siri kwa mnajimu huyo aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa tego lake la nyoka nchini India na kumfanya apate mwaliko katika falme za Kiarabu. Mnajimu huyo ameanika namba zake za simu ili iwe rahisi kwa mtu yeyote kumfuata na kufanya naye mawasiliano, anapatikana kwa 0715281162, Chifu Panduka pia anatibu magonjwa mbalimbali na...

MISRI YAHUSISHWA KUJITOA KWA CHAD AFCON

Picha
Na Mwandishi Wetu Misri jana imeifunga Nigeria bao 1-0 na moja kwa moja kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali zijazo za mataifa Afrika zitakazofanyika Gabon, Misri inahitaji pointi moja tu ili wafuzu. Ishu iko hivi, Chad kama ingeendelea kushiriki mashindano hayo uhakika wa Misri kufuzu usingewezekanika kirahisi, lakini kuna taarifa Mapharao hao wameilazimisha Chad ijitoe ili wao wapate mgongo wa kufuzu. Kwani ukiondoa Misri, timu nyingine yenye matumaini ya kufuzu ni Tanzania ambayo ina pointi moja tu, lakini kama itazifunga Misri na Nigeria ndio itaweza kufuzu ila ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano

MKWASSA HAJALIPWA MSHAHARA WAKE TANGU ALIVYOANZA KAZI MWAKA JANA

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwassa bado anazungushwa kulipwa mshahara wake tangia alipoanza jukumu la kuinoa timu hiyo toka mikononi mwa Mart Nooij. Habari ambazo zina uhakika zinasema kocha huyo hajawahi iupokea mshahara wake hata mara moja tangu alipopewa jukumu la kuinoa timu hiyo, hadi sasa Mkwassa anaidai TFF shilingi Milioni 200. Akithibitisha hayo, kocha Mkwassa amesema ni kweli hajalipwa mshahara wake lakini hataki kuzungumzia hilo labda waajili wake ndiyo wazungumzie. Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa amekataa kuzungumzia hilo, lakini waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii Nape Nnauye amesema serikali haihusiki na malipo ya kocha wa timu ya taifa hivyo TFF yenyewe inapaswa kumlipa. Hata hivyo kuna habari kwamba kocha huyo wa Stars anatamani kurejea katika klabu yake ya zamani ya Yanga Sc ambayo kwa sasa nafasi yake ilishazibwa na Juma Mwambusi Kocha wa timu ya taifa, Charles Boniface Mkwassa hh...

YANGA YAIWINDA VIKALI NDANDA, KAGERA SUGAR WAJIANDAE

Picha
Na Ikram Khamees Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc wameingia kambini jana kwenye hoteli moja ya kifahari na wakijifua kwenye uwanja wa chuo cha ustawi wa jamii Kurasini tayari kabisa kujiandaa na mchezo wake wa kesho dhidi ya Ndanda Fc. Yanga kesho jioni itacheza na Ndanda Fc katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam mchezo wa robo fainali kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kombe la FA. Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Yanga itashuka tena uwanja wa Taifa Aprili 3 kukwaruzana na Kagera Sugar mchezo wa ligi kuu bara, pia itatelemka tena uwanja huo huo wa Taifa Aprili 6 kuvaana na Mtibwa Sugar. Yanga imeamua kuingia kambini kujiandaa na mechi hizo kwani Aprili 9 itacheza na Al Ahly ya Misri mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa barani Afrika Wachezaji wa Yanga wakijifua mbele ya kocha wao Hans Van der Pluijm

AZAM FC WAJIFUA VIKALI, PRISONS WAJIPANGE

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM Kikosi cha mabingwa wa soka ukanda wa Afrika mashariki na kati Azam Fc wanaendelea na mazoezi makali tayari kabisa kabla hawajaifanyia kitu mbaya Prisons ya Mbeya watakapokutana Alhamisi ijayo uwanja wa Azam Complex. Azam na Prisons zitakutana katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, mchezo unaotarajiwa kuanza majira ya saa kumi kamili. Mabingwa hao wa Kagame watakuwa na kazi ngumu kwani kikosi cha Prisons kimekuwa katika wakati mzuri siku za hivi karibuni, Azam pia ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika. Wakiwa mbioni kuelekea katika mchezo wao wa raundi ya pili kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia katika uwanja wao wa Azam, kikosi hicho kimejinasibu kuibuka na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Prisons Wachezaji wa Azam Fc wakiwa mazoezini katika uwanja wao wa Azam Complex, Alhamisi wanakutana na Prisons

MREMBO AMBADILISHA DINI MKOLA MAN, WAZAZI WAKE WAJA JUU

Picha
Na Mwandishi Wetu, TANGA Mwanadada anayefahamika kwa jina la Khadija ambaye ni mwanamitindo inadaiwa anemdatisha kinoma rapa na mtunzi wa nyimbo za 'Multiple Choice', 'Jana na leo' na 'Kitabu' Christopher Mhenga a k a Mkola Man mpaka kufikia kubadilisha dini yake ya ukristo na kuhamia uislamu. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa msanii huyo, amedai Mkola Man haambiwi wala hasikii kwa mwanamke huyo na inadaiwa yuko mbioni kumuoa. Rafiki huyo ambaye amekataa kutaja jina lake, ameongeza kuwa Mkola Man amebadili dini na sasa ni muislamu anaitwa Mustapha, pia rafiki huyo amedai wazazi wa Mkola Man wamezipata habari hizo za mtoto wao kubadili dini ambapo wamemjia juu. Wazazi hao wa Mkola Man ni walokole na wameshitushwa na kitendo cha kijana wao kuhamia uislamu lakini wamesema ni uamuzi wake mwenyewe kupenda anapopenda, kuhusu mahusiano kati ya mtoto wao na mrembo huyo, wazazi hao wamemtaka awe mwangalifu kwani wanawake wa sasa wengi wao ni waongo. "Wanawake wa...

SIMBA YAMLILIA ABEL DHAIRA

Picha
Na Hajji Manara, DAR ES SALAAM Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba wa mchezaji wake wa zamani Abel Dhaira. Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mitandao mikubwa ya nchi hiyo ikiwemo ya gazeti mashuhuri nchini humo New Vision. Mchezaji huyo aliyekuwa akichezea nafasi ya golikipa na ambae alipata pia kuichezea timu ya Taifa ya Uganda alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ya utumbo. Kwetu sisi ni pigo kubwa sana na ni msiba mzito sana ambao umetufanya tupate fadhaa kubwa lakini hatuna la kufanya zaidi ya kumtakia mapumziko mema ya milele. Dhaira anakumbukwa sana na wana-Simba hasa kwa uwezo wake wa kudaka krosi na nidhamu yake iliyokuwa mfano kwa wachezaji wote waliokuwepo kipindi kile. Tunawaomba familia ya marehemu iwe na subira kwenye kipindi hiki kigumu sana kwao Imetolewa na Haji S Manara Mkuu wa Habari Simba Sports Club

MAONI: KIMAHESABU YANGA NA AZAM ZIMESHATOLEWA CAF

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM KWANZA naanza na hii ya kutofanyika kwa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa Afrika kati ya Tanzania na Chad ambao ulikuwa uchezwe leo Machi 28 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Ina maana CAF itaifungia Chad na kuitoza faini, vilevile matokeo yake yote kufutwa, hivyo Tanzania itabakiwa na pointi yake moja, huku Misri ikiendelea kuwa kinara na pointi nne. Itakuwa ngumu tena Tanzania kufuzu kwenye kundi G kwani limesaliwa na timu tatu na litakosa nafasi ya kutoa 'Best Rooser' na kuinyima nafasi nchi yetu kufuzu kwa mara ya pili fainali hizo za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Gabon. WAWAKILISHI WENGINE WA TANZANIA NAO SHAKANI. Tanzania ina wawakilishi wengine wawili katika mashindano ya vilabu barani Afrika, wawakilishi hao ni Yanga Sc na Azam Fc. Yanga Sc inashiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakati Azam Fc inashiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, timu zote hizo zimetinga raundi ya pili na zote zinakabiliwa na ...

CAF YAIFUNGIA CHAD HADI 2021

Picha
Na Mwandishi Wetu Shilikisho la Soka Barani Africa, CAF imetangaza kuifungia nchi ya Chad kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa, AFCON mpaka mwaka 2021 na kuipiga faini ya dola 20,000 kwa kujitoa michuano ya AFCON 2017, hivyo itafungiwa AFCON 2019. Kutokana na kujitoa kwao, mechi yao ya Jumatatu March 28, 2016 dhidi ya Tanzania haitokuwepo tena. Na kwa mujibu wa kanuni za mashindano za CAF, timu itakayojitoa kwenye kundi hatua ya kufuzu, basi matokeo yake yote yatafutwa. Matokeo ya ushindi wa 1-0 waliopata Tanzania kule ugenini yamefutwa na Tanzania sasa itabaki kuwa na point 1 tu. Kwa maana nyingine, kinara wa kundi G pekee ndio atafuzu AFCON 2017 tofauti na awali ambapo timu ya pili ingefuzu mtoano.

CHAD WAIKACHA STARS, WAJITOA MAZIMA

Picha
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM Timu ya taifa ya Chad imejitoa moja kwa moja kwenye michuano ya kufuzu fainali za mataifa Afrika na haitacheza mchezo wake dhidi ya Stars uliopangwa kufanyika kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chad wameandika ya kujitoa na kuituma CAF leo ambapo inasema kuwa wamejitoa moja kwa moja kwenye michuano ya CAF. Hata hivyo hajajulikana chanzo halisi cha kujitoa mashindanoni ingawa Mambo Uwanjani inafahamu kwamba kipigo walichokipata nyumbani kwao N'Djamena dhidi ya Stars ndicho kilichowakatisha tamaa na kusitisha mpango wao wa kurudiana na Stars. Kwa maana hiyo Stars itapewe pointi tatu na magoli matatu na hivyo itafufua matumaini ya Stars kufuzu fainali zijazo za mataifa Afrika zitakazofanyika Gabon

KIPA WA SIMBA AFARIKI DUNIA ICELAND

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM Kipa wa zamani wa Simba Sc Abel Dhaira raia wa Uganda amefariki dunia leo nchini Iceland alikokuwa anacheza soka la kulipwa. Dhaira aliyesajiliwa na Simba ya Tanzania akitokea Uganda alikong'ara na timu ya taifa ya Uganda, The Clanes ameaga dunia baada ya kuugua maradhi ya saratani ya utumbo. Kipa huyo kwa muda sasa alikuwa mgonjwa na taarifa zake zilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ule wa nchini Uganda wa Kawowo.com. Leo mlinda mlango huyo ameaga dunia, mwenyezi mungu aiweke roho yake peponi, Amina

MAJALIWA MGENI RASMI STARS VS CHAD JIMATATU TAIFA, KIINGILIO MKONO WAKO

Picha
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe Majaliwa Kassim Majaliwa anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa mchujo mataifa Afrika kati ya Taifa Stars na Chad uwanja waTaifa Dar es Salaam. Mchezo wa marudiano utakaopigwa jumatatu, unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo Stars ilishinda 1-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika mwakani Gabon.  Shirikisho la kandanda nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo huo ambapo shilingi 5000 tu sawa na mkono mmoja wa mwanadamu wenye vidole vitano vinatosha kukupeleka Taifa kuziona Stars na Chad. Katika mchezo huo wa marudiano Taifa Stars inahitaji ushindi ili ijiwekee mazingira mazuri ya kufuzu kwani Misri na Nigeria zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wao uliofanyika jumatano iliyopita. Waziri mkuu mhe Majaliwa Kasimu Majaliwa, atakuwa mgeni rasmi jumatatu

YANGA, AZAM WABISHA HODI TFF KUTAKA VIPOLO VYA VISOGEZWE MBELE

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc na mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc zimebisha hodi shirikisho la soka nchini TFF kutaka mechi zao za vipolo za ligi kuu bara zisogezwe mbele ili kupata muda wa kujiandaa na mechi zao za kimataifa. Yanga Sc inatarajia kucheza mechi yake ya ligi ya mabingwa barani Afrika raundi ya pili dhidi ya Al Ahly ya Misri ambapo Bodi ya ligi kuu imewapangia mechi zake za vipolo mfululizo. Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga Jerry Muro amedai Yanga imepangiwa ratiba ngumu mno kwani watalazimika kucheza mechi nne mfululizo huku wakikosa kujiandaa kucheza mechi yake na Al Ahly. Azam nao wamepangiwa vipolo vyao kwa ukaribu mno hivyo vitaathili ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa, Azam itakutana na Esperance ya Tunisia kati ya tarehe 10 na 20 au 21 mwezi ujao. Msemaji wa Azam Jaffar Idd  Maganga amesikika akilaani ratiba hiyo na tayari wameshapeleka barua yao TFF kutaka wasogezewe mbele vipolo vyao ama sivyo ushiriki wao kimat...

STAA WETU: BATAROKOTA, ANA VIPAJI VINGI VYA KUJIVUNIA, NDIYE ALIYEITENGENEZA BLOGU HII

Picha
Na Salum Fikiri Jr, MOROGORO Nilisafiri hadi mjini Morogoro maeneo ya Kihonda ili nikutane na jamaa mmoja anayafahamika kwa jina la Paschal Linda ama waweza kumuita Batarokota. Unaweza kujiuliza maswali mara mbili mbili hasa nilipotaja jina la Batarokota ambalo si geni masikioni na machoni kwenu, jina hili lilichomoza mwaka juzi kwenye tuzo za Kill Music Awards 2014 ambazo zilimwezesha msanii Diamond Platinumz kuzoa tuzo saba kwa mkupuo. Batarokota alikuwemo katika tuzo hizo baada ya kuteuliwa kuingia kwenye kategoli, Batarokota alipata nafasi ya kuingia kwenye tuzo hizo na wimbo wake wa 'Kwejaga nyangisha' ambao ni wa asili na ameuimba kwa lugha ya Kisukuma. Kwa bahati mbaya Batarokota hakupata tuzo ila aliweza kujitambulisha vema kwenye medani ya muziki kwani wasanii wengi tu hapa nchini wenye majina makubwa hawakuwahi kuingia kwenye tuzo hizo. Awali Batarokota alikuwa akiimba hip hop na alibahatika kurekodi nyimbo nne ambazo zote ameziweka Youtube hivyo ukizihitaji unawez...

KIKWETE AMLILIA CLUYFF

Picha
Na Mwandishi Wetu, TUNISIA RAIS mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha masikitiko yake na kumlilia gwiji wa zamani wa Barcelona, PSV na timu ya taifa ya Uholanzi Johan Cluyff ambaye amefariki dunia jana kwa naradhi ya saratani. Kikwete ambaye aliwahi kuzawadiwa jezi na gwiji huyo aliyezaliwa mwaka 1945, Rais mstaafu Kikwete alitoa salamu hizo za pole akiwa mjini Tunis alipokuwa kikazi. Kikwete ni mwakilishi maalum wa Umoja wa Afrika katika upatanishi wa nchi ya Libya iliyoingia kwenye mgogoro hasa baada ya kuuawa kwa kiongozi wao Muamar Gaddaf ambapo amani haijapatikana hadi sasa. Katika uongozi wake, Kikwete alikuwa mpenda michezo hasa soka ambapo aliwezesha ziara za klabu kubwa duniani za Real Madrid na Barcelona zote za Hispania ambapo Cluyff naye alibahatika kutua Tanzania na kualikwa Ikulu ya Magogoni na mheshimiwa JK (Picha chini raisi mstaafu Jakaya Kkwete akikabidhiwa jezi ya Barcelona na Johan Cluyff sasa marehemu, Picha kwa hisani ya Ikulu)

UKWELI KUHUSU JKT KANEMBWA NA GEITA GOLD HUU HAPA, TFF WANAPEPESA

Picha
Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM Ukweli ni kwamba JKT Kanembwa ya Kigoma tayari ilikuwa ishatelemka daraja, kwahiyo ikaamua kuvunja kambi yake na kuwaruhusu wachezaji wake kurejea makwao, ina maana hata mchezo wao wa mwisho na Geita Gold wasingeingia uwanjani. Lakini siku ya mchezo wao na Geita Gold chapu chapu viongozi wa Kanembwa waliwapigia simu wachezaji wao ili warejee klabu kwa ajili ya mchezo wao wa mwisho, walipotua tu na kuingia uwanjani wakapokea mabao 8-0 toka kwa wachimba madini wa Geita Gold Mine wanaonolewa na nahodha wa zamani na kocha wa Simba Seleman Matola. TFF inachunguza sakata zima la Geita Gold kuishinda Kanembwa 8-0 na Polisi Tabora kuwachapa JKT Oljoro ya Arusha mabao 7-0, madai yaliyopo mezani kwamba timu hizo zimepanga matokeo. Kama ni kweli timu hizo zilipanga matokeo basi zinaweza kushushwa daraja na kutozwa faini, undani wa sakata hilo TFF wanapepesa macho tu kwani hawajui chochote. Kuna uwezekano mkubwa timu moja kati ya Polisi Tabora au Geita Gold ikapand...

MICHANO: DAZ BABA NAYE ANAHITAJI MSAADA KAMA CHID BENZI

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP...yap...yap...Michano leo inamchana Daz Baba mwanaharakati aliyetumbukia kwenye shimo la madawa ya kulevya, kiukweli amepoteza mwelekeo ingawa kazi ni kazi ila inasikitisha pale anapoendesha maisha yake kwakupiga debe kwenye vituo vya daladala. Huyu jamaa alikuwa kiongozi wa kundi kubwa na maarufu la muziki wa kizazi kipya la Daz Nundaz lenye maskani yake Sinza Dar es Salaam, kundi hilo lilijumuhisha wasanii watano akiwemo yeye. Ila kwa sasa kundi hilo halipo tena yaani kwa maana nyingine limekufa, Daz Nundaz lilijipatia unaarufu mkubwa hasa kwa kuimba nyimbo za huzuni kama Kamanda, Maji ya shingo, Barua na nyinginezo nyingi. Aidha Daz Baba binafsi amepata kutamba na nyimbo zake kama Elimu dunia, Umbo namba 8, Wife, Nipe tano na nyingine, kwa sasa jamaa anahitaji msaada wa kutupiwa kamba ili aishike na atoke kwenye shimo la madawa ya kulevya. Kama mmeweza kumpa kamba Chid Benz basi kamba hiyo mpeni na Daz Baba kiongozi wa zamani wa kundi la Daz Nundaz lililojum...

KITABU CHA MKOLA MAN KIKO TAYARI, PRODYUZA WAKE AANIKA KILA KITU

Picha
Na Mwandishi Wetu Hatimaye rapa mwenye maskani yake Hale mkoani Tanga Mkola Man ameachia wimbo wake mwingine unaokwenda kwa jina la "Kitabu cha historia' ambayo imeshasambazwa kwenye mitandao ya kijamii na redio pia. Akizungumza na mtandao huu, Mkola Man amesema Kitabu kimekamilika na watu kadhaa wameanza kuchangamkia wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wanadownlod kwa wingi. "Nyimbo yangu nimeirekodi katika studio za K.O Record zilizopo hapa Tanga chini ya prodyuza wangu mahiri Mos ambaye yeye ndiye aliyeibua kipaji changu", alisema. Aidha Mwandishi wetu alizungumza na prodyuza wa msanii huyo Mos ambapo alimthibitishia kuwa ngoma yake hiyo iko njema na inafanya vizuri, Mkola Man alitamba na wimbo wake wa kwanza wa "Mr Mapesa" alioutengeneza Mos na kwa sasa msanii huyo anaandika "Michano" kupitia blogu hii, Big up Mkola Man

SAMATTA AWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU MLIPUKO WA MABOMU UBELGIJI

Picha
Na Elias John, D'jamena Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Ali Samatta amewatoa hofu ndugu zake na Watanzania kwa ujumla kuhusu milipuko ya mabomu iliyotokea mjini Brusseils Ubelgiji. Samatta ambaye anachezea KRC Genk ya Ubelgiji hakuwepo kabisa nchini Ubelgiji wakati milipukp hiyo ilipotokea, milipuko hiyo ilitokea juzi jumanne wakati mchezaji huyo tayari alikuwa mjini D'jamena na timu ya taifa. Akizungumza na Mambo Uwanjani mara baada ya kumalizika mchezo kati ya Tanzania na Chad, ambapo Tanzania ilishinda 1-0 huku mfungaji wa bao pekee la Tanzania akiwa ni yeye, Samatta amesema yeye hakuwepo kabisa hivyo ni ngumu kuandika habari kuwa alinusurika. Gazeti moja la michezo nchini Tanzania (Jina tunalo) liliandika Mbwana Samatta alinusurika katika milipuko hiyo ya mabomu jambo ambalo lilizua utata kwa ndugu zake, jamaa na marafiki. "Sikuwepo kabisa Ubelgiji, niko hapa D'jamena tangu jumatatu na milipuko imetokea jumanne ni jambo l...

TANZANIA YAUA CHAD 1-0, SAMATTA ATIMIZA AHADI

Picha
Na Elias John, D'jamena Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo inetimiza ahadi baada ya kuwachapa wenyeji wao Chad bao 1-0 katika uwanja wa Amnisports Idris Mahamat Ouya mjini D'jamena mchezo wa mchujo mataifa barani Afrika. Mbwana Ali Samatta ndiye muuaji wa Chad katika mchezo huo kunako dakika ya 30 kipindi cha kwanza, ushindi huo wa leo unaifanya Stars ifikishe pointi 4 ikiwa imecheza mech tatu, Stars ilianza kwa kuchapwa mabao 3-0 na Misri jijini Cairo kabla haijatoka suluhu na Nigeria uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Stars itarudiana na Chad jumatatu ijayo katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, katika mchezo wa leo, Stars ilicheza vizuri lakini katika dakika za mwisho mwisho vijana wa Chad walilishambulia lango la Stars na almanusura wasawazishe, kiungo wa Stars Mwinyi Kazimoto alitoka nje baada ya kuumia Awali nahodha wa Stars Mbwana Samatta ambaye pia ni mchezaji wa KRC Genk ya Ubelgiji alitamba kuchomoza na ushindi katika mchezo huo wa leo, Samatta alisema ...

'NDI NDI NDI' YAMTOA TENA PANGONI LADY JAYDEE

Picha
Na Prince Hoza Baada ya kimya kingi hatimaye msanii Judith Wambura " Lady Jaydee" amefanikiwa kuachia wimbo wimbo uitwao 'Ndi ndi ndi' na tayari upo mtaani. Jaydee ambaye anafahamika kwa majina kadhaa kama binti Machozi na Komandoo anatazamiwa kufanya uzinduzi mkubwa wa wimbo huo hivi karibuni katika kiwanja chake mwenyewe anachokimiliki. Mwanadada huyo aliyepata kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo Yahaya, ametamba kutamba na wimbo huo mpya unaopatikana mitaani, pia unaweza kuupata wimbo huo kupitia Mkito.com. Lady Jaydee ni mke wa zamani wa mtangazaji maarufu wa E Fm Gadner G Habash, msanii huyo hivi karibuni alizungumzia ujio wake mpya, ambapo pia alidai yeye kamwe hawezi kupotea kwenye muziki kwavile anapata sapota kubwa toka kwa mashabiki wake

TUNAWACHAPA KWAO CHAD- SAMATTA

Picha
Na Elias John, D'jamena Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa, Taifa Stars Mbwana Samatta amewaahidi ushindi Watanzania dhidi ya Chad mchezo wa kufuzu fainali za mataifa Afrika utakaofanyika Jumatano katika uwanja wa Amnisports Idris Mahamat Ouya. Nahodha huyo wa Tanzania aliyekabidhiwa mikoba hiyo hivi karibuni akichukua nafasi ya Nadir Ali "Cannavaro" ametamba ni lazima waibuke na ushindi katika mchezo wa leo licha kwamba wanacheza ugenini. Samatta amedai Tanzania inahitaji kufuzu fainali za mataifa Afrika hivyo hawatakubali iupoteza, aidha pia amedai hiyo haitakuwa kazi nyepesi bali wanahitaji kujituma kwa nguvu zao zote. Stars inayonolewa na Charles Boniface Mkwassa leo jioni itatelemka dimbani kukwaruzana na wenyeji wao Chad ambao pia watarudiana junatatu ijayo jijini Dar es Salaam. Hadi sasa Stars ina pointi moja ikiwa imecheza mechi mbili, moja ikichapwa mabao 3-0 na Misri wakati nyingine ikitoka suluhu na Nigeria 0-0, mchezo wa leo utakuwa mkali kwakuwa kila t...

HIVI UNAJUA KAMA HAMISI KIIZA KAVUNJA REKODI ZOTE ZA TAMBWE KASORO MOJA TU

Picha
Na Ikram Khamees Mshambuliaji wa Simba Mganda Hamisi Friday Kiiza ama Diego ni noma sana kwani msimu wake wa kwanza akiwa na Simba ameweza kuvunja rekodi zote za mshambuliaji mwenzake Amissi Tambwe wa Yanga ambaye pia aliwahi kucheza Simba. Unajua rekodi ngapi alizovunja Kiiza! Hamisi Kiiza kwa sasa amefikisha magoli 19 ambayo yalimpa ufungaji bora Amissi Tambwe mwaka 2013 alipokuwa Simba Sc. Pia Kiiza amezivunja rekodi mbili za Tambwe, Kiiza ameshayavuka magoli 14 ambayo Tambwe aliyafunga msimu uliopita alipokuwa Yanga, pia Kiiza ameshafunga magoli matatu (Hat trick) akiwa na Simba. Bado rekodi moja tu ya kufunga magoli manne kwenye mechi moja, pia Kiiza anaweza akawa hajamfikia Tambwe, kwani mshambuliaji huyo raia wa Burundi ana rekodi ya kuzifunga Simba na Yanga. Lakini muda bado unaruhusu ngoja tuone lolote linaweza kutokea na Tambwe anaweza kumvuka Kiiza ama Kiiza anaweza kuifunga Yanga ili asawazishe rekodi

BANDA, ISIHAKA WAIPASUA KICHWA SIMBA, MAYANJA AFUNGUKA MAZITO

Picha
Na Saida Salum Vitendo vya utovu wa nidhamu vnaendelea kuipasua kichwa klabu ya Simba hasa baada ya wachezaji wake wawili kudaiwa kumtolea lugha chafu kocha mkuu wa timu hiyo Mganda Jackson Mayanja. Mabeki Hassan Isihaka na Abdi Banda wanatajwa kuipasua kichwa Simba na hasa wakiwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu hao wa Msimbazi. Alianza Hassan Isihaka kumchefua Mayanja ambapo mchezaji huyo alikataa kupangwa kwenye mchezo wa kombe la FA kati ya Simba na Singida United. Isihaka alimtolea maneno ya kifedhuli kocha wake Mayanja kwa kudiriki kumpanga kwenye mchezo huo na kumweka benchi kwenye mechi dhidi ya Yanga. Hata hivyo beki huyo ambaye pia alikuwa nahodha wa Simba ameshushwa cheo na kupewa kiungo Jonas Mkude pia akifungiwa mwezi mmoja na kupewa nusu mshahara. Abdi Banda ambaye katika mechi ya watani Simba na Yanga alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya mashabiki wa Simba kumlaumu mwamuzi Jonesia Rukyaa, naye ameonyesha dharau kwa Mayanja na kukataa kuchezeshwa dakik...

BABU LIEWIG ASUKIWA ZENGWE LA KUTIMULIWA STAND UNITED

Picha
Na Pasckal Beatus, Shinyanga Matajiri wa Stand United Acasia wako mbioni kumtupia virago kocha wao mkuu Mfaransa Patrick Liewig "Babu" hasa baada ya mwenendo mbaya wa timu hiyo. Taarifa zenye uhakika kutoka kwa uongozi wa juu wa matajiri hao zinasema Liewig hana muda wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho  kwani matokeo mabovu ndio sababu itakayomuondoa. Kocha huyo alipewa mechi nne tu na aliambiwa kama itapoteza mechi zote hizo basi atafukuzwa, timu hiyo imefanya vibaya katika mechi zake hizo nne hivyo hawaoni sababu ya kuendelea kufanya naye kazi. Pia kocha huyo amekuwa haelewani vizuri na baadhi ya wachezaji wake akiwemo straika aliyekuja vizuri Elius Maguri ambaye aling' ara mwanzoni mwa msimu huu na kupelekea kuitwa timu ya taifa, Taifa Stars. Kwa sasa Maguri amepoteza namba katika kikosi cha timu hiyo na kumfanya ashindwe kutupia magoli kama mzunguko wa kwanza wa ligi ambapo alifunga mabao 9 na kuongoza kwa ufungaji, Liewig aliwahi pia kuinoa Simba Sc msimu w...

STARS WAJIFUA VIKALI D'JAMENA, MKWASSA AAHIDI USHINDI UGENINI

Picha
Na Elias John, D'jamena Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo kimejifua vikali katika uwanja wa Amnisports Idris Mahanat uliopo hapa D'jamena na kwa mara ya kwanza nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta aliwaongoza wenzake. Stars itashuka dimbani jumatano ijayo kukabiliana na wenyeji wao Chad mchezo wa mchujo mataifa barani Afrika. Kocha mkuu wa Stars Charles Boniface Mkwassa amewaahidi Watanzania kwamba atachomoza na ushindi katika mchezo huo ambao unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua. Mkwassa amedai anataka kiwashangaza Watanzania kwa kupata ushindi wa ugenini kama ilivyokuwa kwa vilabu vya Yanga na Azam ambavyo vyote vilishinda katika mechi zao za mashindano ya Afrika. Nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji naye amewataka Watanzania kuwaombea dua ili waweze kufanya vizuri, Stars na Chad zinatarajia kurudiana mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam

MAONI: SIMBA ITANUFAIKA NA VIPOLO VYA YANGA NA AZAM

Picha
Na Prince Hoza Kwanza ningeanza kwa kuzipongeza timu za Yanga na Azam kwa ushindi wao walioupata katika michuano ya kimataifa na kuiwakilisha vema nchi yetu ya Tanzania. Yanga iliifungasha virago APR ya Rwanda kwa kuifunga jumla ya mabao 3-2, Azam nayo imeitoa Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3, sasa timu hizo zimetinga raundi ya pili. Kwenye mada yangu ya leo naizungumzia klabu ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam, hivi karibuni uongozi wa Simba ulitishia kutoingiza timu uwanjani mpaka pale Yanga na Azam zitakapocheza mechi zake za ligi ili kusiwepo na vipolo. Yanga na Azam wana vipolo vya mechi tatu dhidi ya Simba ambayo hadi sasa imecheza mechi 24 huku Yanga na Azam zimecheza mechi 21, Simba wametishia kugoma na wakiitaka TFF kuzipangia mechi Yanga na Azam ili zikamilishe vipolo vyao. Yanga na Azam zimeshindwa kucheza mechi zake za ligi kwakuwa zibabanwa na ratiba ya michuano ya kimataifa, Yanga inawakilisha taifa ikishiri...

AZAM FC YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO

Picha
Na Prince Hoza Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuilaza Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3. Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, Azam Fc ilijipatia ushindi huo na kufanya iwe imeitoa timu hiyo inayomilikiwa na chuo kikuu cha Bidvest jumla ya mabao 7-3 baada ya ushindi wa mabao 3-0 ugenini. Katika mchezo wa leo Azam Fc ilijipatia mabao yake hayo yakifungwa kwa ustadi mkubwa na Kipre Tchetche aliyefunga mabao matatu peke yake 'Hat trick' na lingine la John Raphael Bocco. Magoli ya Bidvest yametiwa kambani na Jabulani Shongwe, Mosiatlhaga Koiekantse na Botes Henrico, Azam sasa imefuzu raundi ya pili na itacheza na Esperance ya Tunisia katika mchezo ujao mwezi Aprili mwaka huu

YANGA SASA USO KWA USO NA AL AHLY APRILI 9

Picha
Na Prince Hoza Hatimaye wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc itakutana na National Al Ahly ya Misri katika hatua ya kuelekea 16 bora. Yanga imetinga raundi ya pili baada ya kuitoa mashindanoni jana APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, Yanga ilishinda mchezo wa kwanza ugenini mabao 2-1 na kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam jana. Al Ahly nao walilazimisha sare ya ugenini dhidi ya Reacreative Libolo ya Angola ya 0-0 kisha kushinda 1-0 mjini Cairo, kwa matokeo hayo sasa Yanga itachuana na Al Ahly mchezo wa kwanza ukipangwa kuanzia jijini Dar es Salaam na wiki moja baadaye zitarudiana Misri. Yanga ina kumbukumbu nzuri ya kushinda 1-0 jijini Dar es Salaam goli likifungwa na nahodha wake Nadir Haroub 'Cannavaro', ila ikafungwa 1-0 ziliporudiana Alexandria. Yanga iliondoshwa kwa matuta 4-3 na hata hivyo Yanga yenyewe ilijilaumu baada ya kukosa penalti ya mwisho ambayo ingewapa ushindi

AZAM KIURAHINI LEO KUTINGA 16 BORA KOMBE LA SHIRIKISHO

Picha
Na Mrisho Hassan Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azam Fc jioni ya leo wanajitupa uwanja wao wa Azam Complex uliopo Chamazi kurudiana na Bidvest Wits ya Afrika Kusini. Azam inahitaji sare ya aina yoyote katika mchezo huo kwani ilijipatia ushindi mnono wa mabao 3-0 ugenini huko Afrika Kusini. Shukrani kwa mabao ya Shomari Kapombe, Kipre Tchetche na nahodha John Raphael Bocco, hivyo katika mechi yake ya leo itakuwa na kazi nyepesi ambayo itawavusha hadi hatua ya 16 bora. Lakini vijana wa Bidvest nao wamewasili nchini kwa lengo moja tu ambalo ni kulipiza kisasi, Bidvest siyo timu ya kubeza kwani katika ligi kuu ya Afrika Kusini inashikilia nafasi za juu hivyo lolote linaweza kutokea. Hadi sasa Tanzania imesaliwa na timu mbili katika michuano ya kimataifa ambazo ni Azam na Yanga ambayo jana ilifanikiwa kutinga raundi ya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika

KIIZA, LYANGA WAIPELEKA SIMBA JIRANI NA UBINGWA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Tanga Washambuliaji Hamisi Kiiza "Diego" na Danny Lyanga jioni ya leo wameiwezesha Simba Sc kuchanja mbuga na kukaribia kabisa ubingwa wa bara baada ya kuifungia mabao muhimu Simba ikiichapa Coastal Union mabao 2-0 uwanja wa Mkwakwani Tanga. Simba ikishangiliwa na mashabiki wake ilijipatia mabao hayo moja kila kipindi na ikijiweka katika mazingira mazuri ya kunyakua kikombe cha ligi kuu bara. Ushindi wa leo dhidi ya Wagosi wa kaya unawafanya Simba kufikisha pointi 57 huku ikiwa imecheza mechi 24, mshambuliaji Hamisi Kiiza anakuwa amefikisha magoli 19 ni sawa kama ameifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa yupo Yanga Amissi Tambwe aliyewahi kuwa mfungaji bora kwa kufunga magoli 19

YANGA YATINGA RAUNDI YA PILI AFRIKA

Picha
Na Prince Hoza Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo wamefanikiwa kuvuka hadi raundi ya pili ya ligi ya mabingwa barani Afrika licha ya kulazimishwa sare ya wageni APR ya Rwanda ya kufungana 1-1 uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga ilianza ikiwa kama imezidiwa kwani dakika ya tatu kipindi cha kwanza iliruhusu bao lililofungwa na Erick Lusanga ambaye leo aliihenyesha mno Yanga. Hata hivyo Yanga waliweza kujirekebisha na kucheza kandanda la kuelewana na katika dakika ya 25 kipindi hicho hicho cha kwanza walifanikiwa iusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Donald Ngoma aliyewatoka mabeki wa APR. Hadi mapumziko matokeo no hayo hayo, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kumshambulia mwenzie lakini hakukuwa na goli, Yanga sasa imefuvu raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya ushindi wa 2-1 ilioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Kigali Rwanda. Ina maana Yanga itakutana na Al  Ahly ya Misri kwani katika mchezo wake wa leo dhidi ya Reacreative Libolo ya...

STAA WETU: DONALD NDOMBO NGOMA: MSHAMBULIAJI ANAYEANZISHA MASHAMBULIZI MWENYEWE

Picha
Na Prince Hoza Yanga leo jioni inashuka uwanja wa Taifa Dar es salaam kukabiliana vikali na APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika. Katika mchezo huo utakaoanza saa kumi kamili jioni unatazamiwa kuwa mkali hasa kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Yanga ilitangulia kushinda mabao 2-1 uwanja wa Amahoro mjini Kigali, shukrani kwa Juma Abdul na Thabani Kamusoko ambao ndio wauaji wa APR. Lakini Yanga inajivunia mshambuliaji wake hatari Donald Ndombo Ngoma raia wa Zimbabwe, Ngoma aliyezaliwa Februali 4, 1989 mjini Halale Zimbabwe amekuwa katika kiwango cha juu mno tangia alipojiunga mwanzoni mwa msimu huu. Ngoma alianza kushangaza wakati wa mchezo wake wa kwanza wa kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Donald Ngoma alikuwa akiinyanyasa safu ya ulinzi ya Gor na kupelekea Yanga kujipatia bao la kuongoza lililofungwa naye, Ngoma alifunga goli hilo baada ya juhudi zake binafsi. Utofauti mkubwa umeonekana kati ya ms...

APR ANAKUFA TENA TAIFA- YANGA

Picha
Na Prince Hoza Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc jioni ya leo wanatarajia kurudiana na APR ya Rwanda katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga wana kumbukumbu nzuri ya kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika juma lililopita huko Kigali, Rwanda hivyo leo hii itakuwa na kazi ya kuulinda ushindi huo. Yanga inahitaji sare tu ili iweze kusonga mbele lakini wapinzani wao ambao waliwasili nchini jana nao wanahitaji ushindi ili waweze kuitoa Yanga. APR wanahitaji mabao 2-0 ili wasonge mbele kwahiyo mchezo huo utakuwa mkali kama ule wa kwanza uliopigwa dimba la Amahoro, kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Pluijm amesema timu yake lazima iibuke na ushindi. Anasema Yanga imejipanga kuibuka na ushindi na itawatumia wachezaji wake walewale waliotumika kuiua katika mchezo wa kwanza, hata hivyo Yanga itamkosa beki wake wa pembeni Juma Abdul

SIMBA YAHOFIA HUJUMA TANGA, YAAPA KUIUA COASTAL LEO

Picha
Na Salum Fikiri Jr,, Tanga Wakati kikosi cha Simba kikiwasili juzi mjini Tanga na kufanya mazoezi yake katika uwanja wa Mkwakwani, kimehofia hujuma baada ya kuwapiga stop mashabiki waliokuwa wakija kuitazama. Kikosi hicho kiliendelea kufanya mazoezi pasipo mashabiki na mwandishi wa habari hizi alipojaribu kuuliza kulikoni muwazuie mashabiki wakajibu kuwa wanahofia hujuma. Tanga kumekuwa na hujuma sana na hasa zinapokwenda kucheza Simba au Yanga, Simba leo jioni inakutana na Coastal Union mchezo wa ligi kuu bara. Endapo Simba itashinda mchezo itakuwa inazidi kuziacha nyuma Yanga na Azam, hadi sasa Simba ina pointi 54 lakini imecheza mechi 23 tofauti na wenzao Yanga na Azam wenye 50 ambao wamecheza mechi 21. Wakati Simba ikihofia hujuma za Coastal lakini kocha wa timu hiyo Jackson Mayanja amejinasibu kuchomoza na ushindi, Coastal ikituamia uwanja wa nyumbani imekuwa na bahati nzuri kwani imewahi kuzichapa Yanga 2-0 na Azam 1-0, Ngoja tuone

ETOILE DU SAHEL YATUMBUA JIPU MSIMBAZI, YADAI ILISHATUMA MGAO WA OKWI ZAMANI

Picha
Na Ikram Khamees Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia imeweka wazi kuwa tayari ilishawatumia Simba fedha zao za mauzo ya mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye ilikuwa haijalipa wakati ilipomchukua. Uongozi wa ngazi ya juu wa Etoile imethibitisha kuwa tayari ilishawalipa Simba dola 350 sawa na shilingi milioni 600 za Kitanzania, Hajji Manara msemaji wa klabu ya Simba amethibitisha kuwa tayari Etoile ilishawatumia Email ikiwaelekeza kuwa fedha zao zimeshaingia katika akaunti yao. Lakini hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa Simba aliyewahi kuzungumzia fedha hizo kama zishatumwa na kila mmoja alikuwa kimya. Mambo Uwanjani ina uhakika kuwa fedha za Okwi zilishatumwa tangia mwezi Februali, lakini ukimya wa viongozi wa Simba unaonyesha waziwazi kuna mgawanyiko mkubwa juu ya mgao huo wa Okwi. Emmanuel Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013 lakini Simba haikulipwa mpaka ilipoamua kwenda kushitaki FIFA, kuoatikana kwa fedha hizo kunatengua u...

MICHANO: HAWATOSHEKI NA UKUBWA WA MAJINA YAO, BADO WANAGOMBANIA MAJINA YA WANYAMA

Picha
Na Mkola Man, Tanga Yap...yap...yap..Michano yangu ya leo inawachana chana na kupasua kuhusu kitendo cha wasanii watano wenye majina (Masupa staa) wakubwa ndani na nje ya bongo, wasanii hao kwakweli siwaelewi kabisa maana wanagombania majina ya wanyama wa porini. Hivi karibuni wasanii watatu waligombania jina la mnyama Simba na kila mmoja akidai ni lake, wasanii hao ni Diamond Platinumz, Mr Blue na Afande Sele "Mfalme", wengine wawili wakigombania jina la Mamba. Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya na Shetta ama baba Kayla kila mmoja alikuwa akidai yeye ni mamba, wakati mamba wenyewe wanaishi majini na kamwe sijawahi kusikia au kuona mamba akiitwa Dudubaya au Shetta. Wala sijawahi kuona mnyama simba akiitwa Diamond, Mr Blue au Afande Sele, ila hao wasanii wetu tayari wameshaingia kwenye malumbano ya kugombania haki ya kumiliki jina la mnyama huku majina yao ya kisanii yaliyowapa umaarufu hawatosheki nayo. Mimi binafsi nimehudhunishwa sana na malumbano hayo, watu wanataka kaz...

KAMUSOKO ALAMBA MILIONI MOJA YA VODACOM

Picha
Na Salum Fikiri Jr Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Scara Kamusoko raia wa Zimbabwe amezawadiwa kitita chake cha shilingi milioni moja na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa ligi kuu Tanzania bara. Kamusoko alikabidhiwa mfano wa hundi fedha hizo baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu bara kwa mwezi Desemba mwaka jana. Kuchukua kwa fedha hizo kiungo huyo wa Yanga kunamwongezea nguvu mpya kwani mwishoni mwa wiki hii ataichezea timu yake ya Yanga itakayoshuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kurudiana na APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika. Kamusoko amekuwa katika kiwango kizuri tangia alipojiunga na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani

SIMBA YAIZUIA COASTAL KUMTUMIA MUUAJI WA YANGA, AZAM

Picha
Na Mkola Man, Tanga Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba Sc imeitaka klabu ya Coastal Union ya Tanga kutomtumia kamwe muuaji wa Yanga na Azam, Miraji Adam Seleman. Muuaji huyo anazuiwa kw sababu anaweza kuvuruga furaha ya Wanasimba ambao hadi sasa wanaendelea kufurahia mafanikio ya timu yao iliyo killeleni mwa msimamo mwa ligi ikiwa na pointi 54. Miraji Adam aliwahi kuzitungua Yanga na Azam katika mechi za ligi kuu bara zote zikichezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga. Simba inakutana na Coastal Union jumamosi ijayo katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na ikishinda mechi hiyo itafikisha pointi 57 na itakuwa karibu kabisa na ubingwa. Kwakuwa Miraji Adam ni mchezaji halali wa Simba na alipelekwa kwa mkopo Coastal hivyo katika mechi yao ya jumamosi hawataki kumuona uwanjani

PRINCE HOZA AANIKA UMRI WAKE

Picha
Na Mwandishi Wetu Leo siku ya Alhamisi tarehe 17-3-2016 ni siku muhimu kwa mmiliki na mtendaji mkuu wa tovuti ya Mambo Uwanjani Prince Hoza. Akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake, Hoza anaweka wazi umri wake tofauti na watu wengine ambao wamekuwa wakificha umri wao. Akizungumza na mtandao huu akitokea nyumbani kwake Tabata Dar es Salaam, Hoza amesema kwamba yeye alizaliwa tarehe 17-03-1978 Kongowe wilayani Kibaha mkoani Pwani. Hoza ambaye ni mtoto wa tatu kati ya watoto tisa wa familia ya Salum Mrisho Matua na Zena Hassan Kiure ambao wote hao kwa sasa ni marehemu. Bodi ya utendaji ya Mambo Uwanjani kwa kushirikiana  na wadau wake wa mitandao yao ya kijamii kama Facebook na WhatsAap inamtakia Happy Birthday njema Prince Hoza Matua

SIMBA YALIA NA YANGA, AZAM NA TFF

Picha
Na Saida Salum Klabu ya Simba imeendelea kulalamikia ratiba ya ligi kuu bara inavyopanguliwa kila kukicha ikiwa na malengo ya kuzibeba Yanga na Azam. Hajji Manara msemaji wa klabu hiyo ameishutumu TFF kwa kuonyesha waziwazi kuzibeba Yanga na Azam kwa kuziondolea mechi zake za ligi kuu bara hivyo sasa utakuwa mtihani mkubwa kwao. Simba ibaongoza ligi hiyo kwa kukusanya pointi 54 lakini imeshuka dimbani mara 22 ikiwa ni tofauti ya mechi mbili na Yanga na mechi tatu na Azam. Yanga ina pointi 50 wakati Azam ina pointi 47, kwahiyo kama itacheza na kushinda mechi zake tatu zilizosalia itafikisha pointi 56 na itakuwa imeishusha Simba katika nafasi yake ya kwanza. Yanga nao wakishinda mechi zao mbili watafikisha pointi 56 na wataishusha Simba katika nafasi yake ya kwanza, Manara ameshangazwa na kitendo cha TFF kuzifutia Yanga na Azam mechi zake za ligi zilizopangwa kuchezwa hivi karibuni. Msemaji huyo amedai hakuna ligi yoyote duniani inayosogezwa mbele kwa sababu kuna timu inashiriki mi...

PLUIJM AIWEKEA MTEGO AL AHLY

Picha
Na Salum Fikiri Jr Kocha mkuu wa Yanga Sc Mholanzi Hans Van der Pluijm anewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa lazima APR ya Rwanda ifungashwe virago katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, lakini watakaokuja mbele yao nao lazima wakalishwe. Yanga itarudiana na APR jumamosi ijayo uwanja wa Taifa Dar es Salaam lakini itakuwa na kazi nyepesi kwani itahitaji matokeo ya sare ya aina yoyote. Pia itakuwa na faida ya kucheza uwanja wa nyumbani, Yanga itapata sapota ya mashabiki wake hivyo Pluijm anajiamini mno na kudai watawachapa tena, katika mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Amahoro mjini Kigali, Yanga ilishinda 2-1. Yanga ikivuka hatua hiyo itakutana na mshindi kati ya Al Ahly ya Misri au Recreative Libolo ya Angola, timu hizo zilitoka suluhu 0-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Angola, Yanga inawafahamu vizuri Ahly na iliwakosakosa kuwatoa mwaka juzi kama si Said Bahanuzi kukosa penalti huenda historia ingebadilika. Pluijm anasema Ahly ni wepesi mno kwao kuliko Libo...

GARI LAMBAKISHA DOGO JANJA TIP TOP

Picha
Na Ikram Khamees Msanii chipukizi Dogo Janja sasa ataendelea kusalia katika kundi lake la Tip Top Connection baada ya uongozi wa kundi hilo kumtunukia gari mpya aina ya Benzi. Akipokea zawadi hiyo aliyokabidhiwa na kiongozi wa Tip Top Connection Hamad Ally au Madee, Dogo Janja ameshukuru na kusema anajivunia kuwa msanii wa kundi hilo na ataendelea kufanya nalo kazi. Awali Dogo Janja alitangaza kulihama kundi hilo baada ya kuhitilafiana na kiongozi wa kundi hilo Madee, lakini baada ya kuzawadiwa gari hilo ametangaza mwenyewe atasalia Tip Top. Msanii huyo tayari ameachia Audio na Video ya wimbo wake mpya 'My Life' ambao umeshaanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya runinga, Good Dogo Janjalo