AZAM FC YAPIGA WANAJESHI 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
Mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc jioni ya leo imefanikiwa kuzima ngebe za maafande wa Prisons ya Mbeya baada ya ouwatandika mabao 3-1 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam.
Ushindi huo unawapeleka Azam Fc hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Azam Sports Federation Cup maarufu kama kombe la FA Cup.
Shomari Kapombe aliifungia Azam mabao mawili wakati Hamisi Mcha akifunga moja na kufanya Azam iibuke na ushindi mnono, bao la kufutia machozi la Prisons lilifungwa na mshambuliaji wake hatari Jeremiah Juma Mgunda.
Hata hivyo mchezo huo ulikuwa mkali na wa kusisimua kwani timu hizo zinapokutana huwa zinakamiana sana, mara ya mwisho kukutana ilikuwa jijini Mbeya uwanja wa Sokoine mchezo wa ligi kuu bara ambapo zilitoka sare ya kufungana 1-1