YANGA VS NDANDA TAIFA, AZAM NA PRISONS CHAMAZI, HAPATOSHI LEO FA CUP

Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM

Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc jioni ya leo wanashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikabili Ndanda Fc ya Mtwara mchezo wa robo fainali kombe la Azam Sports Federation Cup au FA Cup.

Mchezo huo unatazamiwa kuanza saa kumi jioni na utakuwa mkali wenye ushindani hasa kila timu ikitaka kucheza nusu fainali, tayari timu ya Mwadui Fc ya mjini Kahama imeshatangulia nusu fainali.

Mwadui ilipata tiketi hiyo baada ya kuilaza Geita Gold ya Geita mabao 3-0, mchezo mwingine unatarajia kufanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi kati ya mabingwa Afrika mashariki na kati maarufu kbe la Kagame Azam Fc itachuana na Prisons ya Mbeya.

Mchezo huo nao utakuwa mkali kutokana na timu hizo kuonyeshana undava kila zinapokutana

Amissi Tambwe wa Yanga akikabiliana vikali na mlinzi wa Ndanda wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA