'NDI NDI NDI' YAMTOA TENA PANGONI LADY JAYDEE
Na Prince Hoza
Baada ya kimya kingi hatimaye msanii Judith Wambura " Lady Jaydee" amefanikiwa kuachia wimbo wimbo uitwao 'Ndi ndi ndi' na tayari upo mtaani.
Jaydee ambaye anafahamika kwa majina kadhaa kama binti Machozi na Komandoo anatazamiwa kufanya uzinduzi mkubwa wa wimbo huo hivi karibuni katika kiwanja chake mwenyewe anachokimiliki.
Mwanadada huyo aliyepata kutamba na nyimbo kadhaa ikiwemo Yahaya, ametamba kutamba na wimbo huo mpya unaopatikana mitaani, pia unaweza kuupata wimbo huo kupitia Mkito.com.
Lady Jaydee ni mke wa zamani wa mtangazaji maarufu wa E Fm Gadner G Habash, msanii huyo hivi karibuni alizungumzia ujio wake mpya, ambapo pia alidai yeye kamwe hawezi kupotea kwenye muziki kwavile anapata sapota kubwa toka kwa mashabiki wake