PRINCE HOZA AANIKA UMRI WAKE
Na Mwandishi Wetu
Leo siku ya Alhamisi tarehe 17-3-2016 ni siku muhimu kwa mmiliki na mtendaji mkuu wa tovuti ya Mambo Uwanjani Prince Hoza.
Akiadhimisha siku ya kuzaliwa kwake, Hoza anaweka wazi umri wake tofauti na watu wengine ambao wamekuwa wakificha umri wao.
Akizungumza na mtandao huu akitokea nyumbani kwake Tabata Dar es Salaam, Hoza amesema kwamba yeye alizaliwa tarehe 17-03-1978 Kongowe wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Hoza ambaye ni mtoto wa tatu kati ya watoto tisa wa familia ya Salum Mrisho Matua na Zena Hassan Kiure ambao wote hao kwa sasa ni marehemu.
Bodi ya utendaji ya Mambo Uwanjani kwa kushirikiana na wadau wake wa mitandao yao ya kijamii kama Facebook na WhatsAap inamtakia Happy Birthday njema Prince Hoza Matua