SIMBA YALIA NA YANGA, AZAM NA TFF
Na Saida Salum
Klabu ya Simba imeendelea kulalamikia ratiba ya ligi kuu bara inavyopanguliwa kila kukicha ikiwa na malengo ya kuzibeba Yanga na Azam.
Hajji Manara msemaji wa klabu hiyo ameishutumu TFF kwa kuonyesha waziwazi kuzibeba Yanga na Azam kwa kuziondolea mechi zake za ligi kuu bara hivyo sasa utakuwa mtihani mkubwa kwao.
Simba ibaongoza ligi hiyo kwa kukusanya pointi 54 lakini imeshuka dimbani mara 22 ikiwa ni tofauti ya mechi mbili na Yanga na mechi tatu na Azam.
Yanga ina pointi 50 wakati Azam ina pointi 47, kwahiyo kama itacheza na kushinda mechi zake tatu zilizosalia itafikisha pointi 56 na itakuwa imeishusha Simba katika nafasi yake ya kwanza.
Yanga nao wakishinda mechi zao mbili watafikisha pointi 56 na wataishusha Simba katika nafasi yake ya kwanza, Manara ameshangazwa na kitendo cha TFF kuzifutia Yanga na Azam mechi zake za ligi zilizopangwa kuchezwa hivi karibuni.
Msemaji huyo amedai hakuna ligi yoyote duniani inayosogezwa mbele kwa sababu kuna timu inashiriki michuano ya kimataifa, ameongeza kuwa hiyo ipo hapa Tanzania pekee na si kwingineko.
Hata hivyo Manara amedai hiyo ni mbeleko ya kuzibeba Yanga na Azam, Yanga haitacheza tena ligi mwezi huu na itasubiri hadi mwezi ujao, wakati Azam itacheza mchezo mmoja tu kisha itasubiri hadi mwezi ujao.
Simba itatelemka tena uwanjani siku ya jumamosi katika dimba la Mkwakwani Tanga kuwavaa Coastal Union ambao ni wababe wa Yanga na Azam, vigogo hivyo vyote vililala kwa Wagosi hao wa Kaya.
Yanga ilifungwa mabao 2-0 wakati Azam ilichapwa 1-0 na kuweza kutibua kasi yao ya kuelekea kwenye ubingwa