APR ANAKUFA TENA TAIFA- YANGA
Na Prince Hoza
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Yanga Sc jioni ya leo wanatarajia kurudiana na APR ya Rwanda katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga wana kumbukumbu nzuri ya kushinda 2-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika juma lililopita huko Kigali, Rwanda hivyo leo hii itakuwa na kazi ya kuulinda ushindi huo.
Yanga inahitaji sare tu ili iweze kusonga mbele lakini wapinzani wao ambao waliwasili nchini jana nao wanahitaji ushindi ili waweze kuitoa Yanga.
APR wanahitaji mabao 2-0 ili wasonge mbele kwahiyo mchezo huo utakuwa mkali kama ule wa kwanza uliopigwa dimba la Amahoro, kocha mkuu wa Yanga Mholanzi Hans Pluijm amesema timu yake lazima iibuke na ushindi.
Anasema Yanga imejipanga kuibuka na ushindi na itawatumia wachezaji wake walewale waliotumika kuiua katika mchezo wa kwanza, hata hivyo Yanga itamkosa beki wake wa pembeni Juma Abdul