TANZANIA YAUA CHAD 1-0, SAMATTA ATIMIZA AHADI
Na Elias John, D'jamena
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo inetimiza ahadi baada ya kuwachapa wenyeji wao Chad bao 1-0 katika uwanja wa Amnisports Idris Mahamat Ouya mjini D'jamena mchezo wa mchujo mataifa barani Afrika.
Mbwana Ali Samatta ndiye muuaji wa Chad katika mchezo huo kunako dakika ya 30 kipindi cha kwanza, ushindi huo wa leo unaifanya Stars ifikishe pointi 4 ikiwa imecheza mech tatu, Stars ilianza kwa kuchapwa mabao 3-0 na Misri jijini Cairo kabla haijatoka suluhu na Nigeria uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Stars itarudiana na Chad jumatatu ijayo katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam, katika mchezo wa leo, Stars ilicheza vizuri lakini katika dakika za mwisho mwisho vijana wa Chad walilishambulia lango la Stars na almanusura wasawazishe, kiungo wa Stars Mwinyi Kazimoto alitoka nje baada ya kuumia
Awali nahodha wa Stars Mbwana Samatta ambaye pia ni mchezaji wa KRC Genk ya Ubelgiji alitamba kuchomoza na ushindi katika mchezo huo wa leo, Samatta alisema ni lazima washinde kwani wamedhamilia kufanya hivyo na ni kweli ahadi imetimia