HIVI UNAJUA KAMA HAMISI KIIZA KAVUNJA REKODI ZOTE ZA TAMBWE KASORO MOJA TU
Na Ikram Khamees
Mshambuliaji wa Simba Mganda Hamisi Friday Kiiza ama Diego ni noma sana kwani msimu wake wa kwanza akiwa na Simba ameweza kuvunja rekodi zote za mshambuliaji mwenzake Amissi Tambwe wa Yanga ambaye pia aliwahi kucheza Simba.
Unajua rekodi ngapi alizovunja Kiiza! Hamisi Kiiza kwa sasa amefikisha magoli 19 ambayo yalimpa ufungaji bora Amissi Tambwe mwaka 2013 alipokuwa Simba Sc.
Pia Kiiza amezivunja rekodi mbili za Tambwe, Kiiza ameshayavuka magoli 14 ambayo Tambwe aliyafunga msimu uliopita alipokuwa Yanga, pia Kiiza ameshafunga magoli matatu (Hat trick) akiwa na Simba.
Bado rekodi moja tu ya kufunga magoli manne kwenye mechi moja, pia Kiiza anaweza akawa hajamfikia Tambwe, kwani mshambuliaji huyo raia wa Burundi ana rekodi ya kuzifunga Simba na Yanga.
Lakini muda bado unaruhusu ngoja tuone lolote linaweza kutokea na Tambwe anaweza kumvuka Kiiza ama Kiiza anaweza kuifunga Yanga ili asawazishe rekodi