BANDA, ISIHAKA WAIPASUA KICHWA SIMBA, MAYANJA AFUNGUKA MAZITO
Na Saida Salum
Vitendo vya utovu wa nidhamu vnaendelea kuipasua kichwa klabu ya Simba hasa baada ya wachezaji wake wawili kudaiwa kumtolea lugha chafu kocha mkuu wa timu hiyo Mganda Jackson Mayanja.
Mabeki Hassan Isihaka na Abdi Banda wanatajwa kuipasua kichwa Simba na hasa wakiwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu hao wa Msimbazi.
Alianza Hassan Isihaka kumchefua Mayanja ambapo mchezaji huyo alikataa kupangwa kwenye mchezo wa kombe la FA kati ya Simba na Singida United.
Isihaka alimtolea maneno ya kifedhuli kocha wake Mayanja kwa kudiriki kumpanga kwenye mchezo huo na kumweka benchi kwenye mechi dhidi ya Yanga.
Hata hivyo beki huyo ambaye pia alikuwa nahodha wa Simba ameshushwa cheo na kupewa kiungo Jonas Mkude pia akifungiwa mwezi mmoja na kupewa nusu mshahara.
Abdi Banda ambaye katika mechi ya watani Simba na Yanga alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya mashabiki wa Simba kumlaumu mwamuzi Jonesia Rukyaa, naye ameonyesha dharau kwa Mayanja na kukataa kuchezeshwa dakika chache na kufikia hatua ya kumdhihaki Mayanja.
Hata hivyo Mayanja amefunguka na kudai hakuna mchezaji aliyejuu ya klabu, hivyo Banda atabakia kuwa Banda na Simba itaendelea kuwa Simba.
Kwa kauli hiyo ya Mayanja ina maaba mchezaji huyo ataendelea kusugua benchi mpaka pale atakapomwomba radhi