SIMBA YAMLILIA ABEL DHAIRA
Na Hajji Manara, DAR ES SALAAM
Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko taarifa ya msiba wa mchezaji wake wa zamani Abel Dhaira.
Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mitandao mikubwa ya nchi hiyo ikiwemo ya gazeti mashuhuri nchini humo New Vision.
Mchezaji huyo aliyekuwa akichezea nafasi ya golikipa na ambae alipata pia kuichezea timu ya Taifa ya Uganda alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ya utumbo.
Kwetu sisi ni pigo kubwa sana na ni msiba mzito sana ambao umetufanya tupate fadhaa kubwa lakini hatuna la kufanya zaidi ya kumtakia mapumziko mema ya milele.
Dhaira anakumbukwa sana na wana-Simba hasa kwa uwezo wake wa kudaka krosi na nidhamu yake iliyokuwa mfano kwa wachezaji wote waliokuwepo kipindi kile.
Tunawaomba familia ya marehemu iwe na subira kwenye kipindi hiki kigumu sana kwao
Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa Habari Simba Sports Club