AZAM FC YASONGA MBELE KOMBE LA SHIRIKISHO

Na Prince Hoza

Mabingwa wa Afrika mashariki na kati Azam Fc jioni ya leo wamefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuilaza Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa mabao 4-3.

Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, Azam Fc ilijipatia ushindi huo na kufanya iwe imeitoa timu hiyo inayomilikiwa na chuo kikuu cha Bidvest jumla ya mabao 7-3 baada ya ushindi wa mabao 3-0 ugenini.

Katika mchezo wa leo Azam Fc ilijipatia mabao yake hayo yakifungwa kwa ustadi mkubwa na Kipre Tchetche aliyefunga mabao matatu peke yake 'Hat trick' na lingine la John Raphael Bocco.

Magoli ya Bidvest yametiwa kambani na Jabulani Shongwe, Mosiatlhaga Koiekantse na Botes Henrico, Azam sasa imefuzu raundi ya pili na itacheza na Esperance ya Tunisia katika mchezo ujao mwezi Aprili mwaka huu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA