KAMUSOKO ALAMBA MILIONI MOJA YA VODACOM
Na Salum Fikiri Jr
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Thabani Scara Kamusoko raia wa Zimbabwe amezawadiwa kitita chake cha shilingi milioni moja na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ambao ni wadhamini wakuu wa ligi kuu Tanzania bara.
Kamusoko alikabidhiwa mfano wa hundi fedha hizo baada ya kuibuka mchezaji bora wa ligi kuu bara kwa mwezi Desemba mwaka jana.
Kuchukua kwa fedha hizo kiungo huyo wa Yanga kunamwongezea nguvu mpya kwani mwishoni mwa wiki hii ataichezea timu yake ya Yanga itakayoshuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kurudiana na APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kamusoko amekuwa katika kiwango kizuri tangia alipojiunga na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani