GARI LAMBAKISHA DOGO JANJA TIP TOP
Na Ikram Khamees
Msanii chipukizi Dogo Janja sasa ataendelea kusalia katika kundi lake la Tip Top Connection baada ya uongozi wa kundi hilo kumtunukia gari mpya aina ya Benzi.
Akipokea zawadi hiyo aliyokabidhiwa na kiongozi wa Tip Top Connection Hamad Ally au Madee, Dogo Janja ameshukuru na kusema anajivunia kuwa msanii wa kundi hilo na ataendelea kufanya nalo kazi.
Awali Dogo Janja alitangaza kulihama kundi hilo baada ya kuhitilafiana na kiongozi wa kundi hilo Madee, lakini baada ya kuzawadiwa gari hilo ametangaza mwenyewe atasalia Tip Top.
Msanii huyo tayari ameachia Audio na Video ya wimbo wake mpya 'My Life' ambao umeshaanza kurushwa katika vituo mbalimbali vya runinga, Good Dogo Janjalo