STAA WETU: DONALD NDOMBO NGOMA: MSHAMBULIAJI ANAYEANZISHA MASHAMBULIZI MWENYEWE
Na Prince Hoza
Yanga leo jioni inashuka uwanja wa Taifa Dar es salaam kukabiliana vikali na APR ya Rwanda mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
Katika mchezo huo utakaoanza saa kumi kamili jioni unatazamiwa kuwa mkali hasa kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza.
Yanga ilitangulia kushinda mabao 2-1 uwanja wa Amahoro mjini Kigali, shukrani kwa Juma Abdul na Thabani Kamusoko ambao ndio wauaji wa APR.
Lakini Yanga inajivunia mshambuliaji wake hatari Donald Ndombo Ngoma raia wa Zimbabwe, Ngoma aliyezaliwa Februali 4, 1989 mjini Halale Zimbabwe amekuwa katika kiwango cha juu mno tangia alipojiunga mwanzoni mwa msimu huu.
Ngoma alianza kushangaza wakati wa mchezo wake wa kwanza wa kombe la Kagame dhidi ya Gor Mahia ya Kenya mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Donald Ngoma alikuwa akiinyanyasa safu ya ulinzi ya Gor na kupelekea Yanga kujipatia bao la kuongoza lililofungwa naye, Ngoma alifunga goli hilo baada ya juhudi zake binafsi.
Utofauti mkubwa umeonekana kati ya mshambuliaji huyo na wengine waliopo hapa nchini ni mkubwa sana, Ngoma ni mshambuliaji nwenye uwezo mkubwa kwani anaweza kuanzisha mashambulizi yeye mwenyewe na pia akafunga.
Hadi sasa ameshafunga magoli 13 katika msimamo wa ligi kuu bara, lolote linaweza kutokea kwani anaweza kuibuka mfungaji bora mwisho wa siku.
Ngoma anakumbukwa vema na Simba kwani zilipokutana hivi karibuni yeye ndiye aliyewalaza mapema mashabiki wa Simba, katika mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-0 huku yeye ni Amissi Tambwe wakifunga kila mmoja.
Yanga walifikia hatua ya kumsajili Ngoma baada ya kuridhishwa naye, Ngoma alikuwa akiichezea Fc Platinum ya Zimbabwe ambapo timu hiyo ilikutana mwaka jana na Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Ndipo Yanga waliponogewa na soka lake na kuamua kumchukua, mshambuliaji ni mmoja kati ya washambuliaji hatari kabisa kuwahi kutokea hapa nchini na amekuwa akipigiwa hesabu za kuondoka nchini na kwenda kucheza soka la kulipwa ughaibuni
Changamoto nyingine anazopitia mshambuliaji huyo ni kuwindwa na mabeki wa timu pinzani, Ngoma anakaniwa sana na amekuwa akiongoza kwa kuchezewa rafu nyingi.
Hiyo inamfanya Ngoma kuwa na hasira kali na inafikia hatua anapaniki na kurudisha rafu anazochezewa, Ngoma kuna wakati anarusha ngumi na kusababisha kuonyeshwa kadi nyekundu.
Mara yavkwanza alikuwa akionyeshwa sana kadi lakini baada ya kocha wake Hans Van der Plujm kumkalisha kitako, Ngoma amebadilika na sasa arudishii rafu anazochezewa