MAJALIWA MGENI RASMI STARS VS CHAD JIMATATU TAIFA, KIINGILIO MKONO WAKO
Na Mrisho Hassan, DAR ES SALAAM
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe Majaliwa Kassim Majaliwa anatazamiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa mchujo mataifa Afrika kati ya Taifa Stars na Chad uwanja waTaifa Dar es Salaam.
Mchezo wa marudiano utakaopigwa jumatatu, unatazamiwa kuwa mkali na wa kusisimua kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza ambapo Stars ilishinda 1-0 na kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali hizo zitakazofanyika mwakani Gabon.
Shirikisho la kandanda nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo huo ambapo shilingi 5000 tu sawa na mkono mmoja wa mwanadamu wenye vidole vitano vinatosha kukupeleka Taifa kuziona Stars na Chad.
Katika mchezo huo wa marudiano Taifa Stars inahitaji ushindi ili ijiwekee mazingira mazuri ya kufuzu kwani Misri na Nigeria zilitoka sare ya 1-1 katika mchezo wao uliofanyika jumatano iliyopita.