ETOILE DU SAHEL YATUMBUA JIPU MSIMBAZI, YADAI ILISHATUMA MGAO WA OKWI ZAMANI

Na Ikram Khamees

Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia imeweka wazi kuwa tayari ilishawatumia Simba fedha zao za mauzo ya mshambuliaji raia wa Uganda Emmanuel Okwi ambaye ilikuwa haijalipa wakati ilipomchukua.

Uongozi wa ngazi ya juu wa Etoile imethibitisha kuwa tayari ilishawalipa Simba dola 350 sawa na shilingi milioni 600 za Kitanzania, Hajji Manara msemaji wa klabu ya Simba amethibitisha kuwa tayari Etoile ilishawatumia Email ikiwaelekeza kuwa fedha zao zimeshaingia katika akaunti yao.

Lakini hadi sasa hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa Simba aliyewahi kuzungumzia fedha hizo kama zishatumwa na kila mmoja alikuwa kimya.

Mambo Uwanjani ina uhakika kuwa fedha za Okwi zilishatumwa tangia mwezi Februali, lakini ukimya wa viongozi wa Simba unaonyesha waziwazi kuna mgawanyiko mkubwa juu ya mgao huo wa Okwi.

Emmanuel Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia mwaka 2013 lakini Simba haikulipwa mpaka ilipoamua kwenda kushitaki FIFA, kuoatikana kwa fedha hizo kunatengua uvumi uliozagaa kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage ambaye aliambiwa kula hela hizo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA