SIMBA YAIZUIA COASTAL KUMTUMIA MUUAJI WA YANGA, AZAM
Na Mkola Man, Tanga
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba Sc imeitaka klabu ya Coastal Union ya Tanga kutomtumia kamwe muuaji wa Yanga na Azam, Miraji Adam Seleman.
Muuaji huyo anazuiwa kw sababu anaweza kuvuruga furaha ya Wanasimba ambao hadi sasa wanaendelea kufurahia mafanikio ya timu yao iliyo killeleni mwa msimamo mwa ligi ikiwa na pointi 54.
Miraji Adam aliwahi kuzitungua Yanga na Azam katika mechi za ligi kuu bara zote zikichezwa katika uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.
Simba inakutana na Coastal Union jumamosi ijayo katika uwanja wa Mkwakwani Tanga na ikishinda mechi hiyo itafikisha pointi 57 na itakuwa karibu kabisa na ubingwa.
Kwakuwa Miraji Adam ni mchezaji halali wa Simba na alipelekwa kwa mkopo Coastal hivyo katika mechi yao ya jumamosi hawataki kumuona uwanjani