CHAD WAIKACHA STARS, WAJITOA MAZIMA
Na Saida Salum, DAR ES SALAAM
Timu ya taifa ya Chad imejitoa moja kwa moja kwenye michuano ya kufuzu fainali za mataifa Afrika na haitacheza mchezo wake dhidi ya Stars uliopangwa kufanyika kesho uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Chad wameandika ya kujitoa na kuituma CAF leo ambapo inasema kuwa wamejitoa moja kwa moja kwenye michuano ya CAF.
Hata hivyo hajajulikana chanzo halisi cha kujitoa mashindanoni ingawa Mambo Uwanjani inafahamu kwamba kipigo walichokipata nyumbani kwao N'Djamena dhidi ya Stars ndicho kilichowakatisha tamaa na kusitisha mpango wao wa kurudiana na Stars.
Kwa maana hiyo Stars itapewe pointi tatu na magoli matatu na hivyo itafufua matumaini ya Stars kufuzu fainali zijazo za mataifa Afrika zitakazofanyika Gabon