AZAM FC WAJIFUA VIKALI, PRISONS WAJIPANGE
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM
Kikosi cha mabingwa wa soka ukanda wa Afrika mashariki na kati Azam Fc wanaendelea na mazoezi makali tayari kabisa kabla hawajaifanyia kitu mbaya Prisons ya Mbeya watakapokutana Alhamisi ijayo uwanja wa Azam Complex.
Azam na Prisons zitakutana katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, mchezo unaotarajiwa kuanza majira ya saa kumi kamili.
Mabingwa hao wa Kagame watakuwa na kazi ngumu kwani kikosi cha Prisons kimekuwa katika wakati mzuri siku za hivi karibuni, Azam pia ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Wakiwa mbioni kuelekea katika mchezo wao wa raundi ya pili kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia katika uwanja wao wa Azam, kikosi hicho kimejinasibu kuibuka na ushindi katika mchezo huo dhidi ya Prisons