MKWASSA HAJALIPWA MSHAHARA WAKE TANGU ALIVYOANZA KAZI MWAKA JANA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwassa bado anazungushwa kulipwa mshahara wake tangia alipoanza jukumu la kuinoa timu hiyo toka mikononi mwa Mart Nooij.
Habari ambazo zina uhakika zinasema kocha huyo hajawahi iupokea mshahara wake hata mara moja tangu alipopewa jukumu la kuinoa timu hiyo, hadi sasa Mkwassa anaidai TFF shilingi Milioni 200.
Akithibitisha hayo, kocha Mkwassa amesema ni kweli hajalipwa mshahara wake lakini hataki kuzungumzia hilo labda waajili wake ndiyo wazungumzie.
Katibu mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa amekataa kuzungumzia hilo, lakini waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Wasanii Nape Nnauye amesema serikali haihusiki na malipo ya kocha wa timu ya taifa hivyo TFF yenyewe inapaswa kumlipa.
Hata hivyo kuna habari kwamba kocha huyo wa Stars anatamani kurejea katika klabu yake ya zamani ya Yanga Sc ambayo kwa sasa nafasi yake ilishazibwa na Juma Mwambusi