YANGA, AZAM WABISHA HODI TFF KUTAKA VIPOLO VYA VISOGEZWE MBELE

Na Ikram Khamees, DAR ES SALAAM

Mabingwa wa soka nchini Yanga Sc na mabingwa wa kombe la Kagame Azam Fc zimebisha hodi shirikisho la soka nchini TFF kutaka mechi zao za vipolo za ligi kuu bara zisogezwe mbele ili kupata muda wa kujiandaa na mechi zao za kimataifa.

Yanga Sc inatarajia kucheza mechi yake ya ligi ya mabingwa barani Afrika raundi ya pili dhidi ya Al Ahly ya Misri ambapo Bodi ya ligi kuu imewapangia mechi zake za vipolo mfululizo.

Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga Jerry Muro amedai Yanga imepangiwa ratiba ngumu mno kwani watalazimika kucheza mechi nne mfululizo huku wakikosa kujiandaa kucheza mechi yake na Al Ahly.

Azam nao wamepangiwa vipolo vyao kwa ukaribu mno hivyo vitaathili ushiriki wao kwenye michuano ya kimataifa, Azam itakutana na Esperance ya Tunisia kati ya tarehe 10 na 20 au 21 mwezi ujao.

Msemaji wa Azam Jaffar Idd  Maganga amesikika akilaani ratiba hiyo na tayari wameshapeleka barua yao TFF kutaka wasogezewe mbele vipolo vyao ama sivyo ushiriki wao kimataifa hautakuwa na faida yoyote

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA