KIPA WA SIMBA AFARIKI DUNIA ICELAND
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
Kipa wa zamani wa Simba Sc Abel Dhaira raia wa Uganda amefariki dunia leo nchini Iceland alikokuwa anacheza soka la kulipwa.
Dhaira aliyesajiliwa na Simba ya Tanzania akitokea Uganda alikong'ara na timu ya taifa ya Uganda, The Clanes ameaga dunia baada ya kuugua maradhi ya saratani ya utumbo.
Kipa huyo kwa muda sasa alikuwa mgonjwa na taarifa zake zilisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ule wa nchini Uganda wa Kawowo.com.
Leo mlinda mlango huyo ameaga dunia, mwenyezi mungu aiweke roho yake peponi, Amina